Mkutano G20 kufanyika kwa video

Thursday March 26 2020

 

Riyad, Saudia. Kilele cha mkutano wa nchi zenye uchumi mkubwa duniani (G20), kinatarajiwa kufanyika kesho.

Hata hivyo, tofauti na ilivyozoeleka mkutano huo sasa utafanyika kwa njia ya viedo kutokana na tishio la maambukizi ya virusi vya corona (covid-19).

Mfalme Saudia Arabia, Salman bin Abdulaz ambaye ndiyo mwenyekiti wa mkutano huo kwa mwaka 2020 anatarajiwa kuongoza kikao hicho.

Mfalme Salman alisema mkutano huo utatafuta mbinu za pamoja za kupambana na janga hilo ambalo mpaka sasa limesababisha vifo vya zaidi ya watu 21,000 duniani.

Katika taarifa yake mfalme Salman alisema mkutano huo pia utajadili namna ya kunusuru uchumi wa dunia katika kipindi hiki ambako mataifa yameathirika na virusi hivyo.

Mfalme Salman mkutano huo pia utahusisha viongozi wa Hispania, Jordan, Singapor, Uswisi, Umoja wa Mataifa (UN), Benki ya Dunia (WB) na Shirka la Afya Duniani (WHO).

Advertisement

Awali Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres alishauri kuanzishwa kwa  mfuko mkubwa wa kusaidia mapambano dhidi ya coroa.

Katibu Guterres alisema mfuko huo unapasw akuanzishwa na nchi wanachama wa G20 ili kusaidia kupambana na janga la virusi vya corona kwa nchi zisizo na uwezo.

Advertisement