Papa amaliza ziara bara la Asia

Japan. Kiongozi wa Kanisa Katoliki, Papa Francis amekutana na ‘Jamii ya Yesu’ katika siku ya mwisho ya ziara yake barani Asia.

Jamii hiyo inayotambulika na Kanisa Katoliki inapatikana nchini Japan ambako Papa Francis alifanya ziara ya siku nne.

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la BBC, Papa Francis aliendesha misa asubuhi ya leo katika kanisa la jamii hiyo iliyopo katia Chuo Kikuu cha Sophia.

Papa Francis pia aliwatembelea mapadri waliostaafu na wagonjwa kabla ya kutoa hotuba kuhusu elimu ya jamii hiyo ya Yesu katika tukio la mwisho katika ziara yake ya wiki nzima katika mataifa ya Asia.

Inaelezwa kuwa akiwa mtoto Papa Francis ambaye jina lake halisi ni Jorge Mario Bergoglio alikuwa ni miuongoni wa vijana wa jamii hiyo nchini Argentina ambako ndoto yake kuba ilikuwa ni kufuata nyayo za mtakatifu Francis Xavier, ambaye aliiingiza Ukristo nchini Japan katika karne ya 16.

Papa Francis amemaliza ziara yake ya siku nane katika bara la Asia ambako alizitembelea mataifa ya Thailand na Japan kwa siku nne kila moja.