Wananchi walivyozungumzia uamuzi wa Sumaye

Wednesday December 4 2019

Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Frederick

Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Frederick Sumaye akiondoka katika chumba cha mkutano baada ya kutangaza kukihama chama cha Chadema katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Picha na Ericky Boniphace  

By Exaud Mtei, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Baada ya waziri mkuu mstaafu, Frederick Sumaye kueleza uamuzi wake wa kujivua uanachama wa Chadema kwa madai ya kutotendewa haki katika uchaguzi wa uenyekiti wa Kanda ya Pwani, wananchi wamesema ni vyema angeondoka katika chama hicho bila kueleza sababu lukuki.

Katika maoni hayo kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ya Mwananchi, Jimmy p  amesema anamshangaa Sumaye kukaa kimya kuhusu kilichoendelea katika uchaguzi wa kanda hiyo ambao alipigiwa kura 48 za hapana kati ya 76, “mbona hamsemi mapema mpaka mkwame vitu fulani, sasa ungeonja sumu kwa ulimi tungesikia haya,  acha mbwembwe mzee.”

Naye Princeton amesema watu najifunza kutokana na makosa, kwamba waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa aliaminiwa mwisho wa siku aliondoka Chadema na kurejea CCM.

Chris Ambrose amesema, “kwa hiyo target (lengo) yako ilikuwa kumng'oa mwenyekiti? Pole mzee, hapo umechemka, Mbowe (Freeman- mwenyekiti wa Chadema) katoka mbali sana na hiki chama. Sio rahisi kukukubali wewe wa juzi tu kwa sababu walishakustukia mapema lengo lako.”

Abel Isaack amesema, “huyu mzee anazeeka vibaya kwenye siasa huwezi kuwa free agent wa kutumika na kila chama.”

Kwa upande wake Zakia Salim amesema, “alikosa urais akahama CCM, amekosa uenyekiti kanda ya Pwani kahama Chadema. Aende ACT labda atapata uongozi.”

Advertisement

“Baba muungwana akivuliwa nguo huchutama tu.
Haya maneno mengi yanavunja heshima, mwenzio aliondoka kitaratibu sana wewe naye rudi nyumbani taratibu. Suala la rushwa linajulikana linatakiwa kuripotiwa wapi,” amesema

Ahmad A Rajab amesema, “ndio maana tunasema siku zote maneno ya wanasiasa wa Afrika yako mdomoni tu kufurahisha wanaokusikiliza moyoni hayapo.”

“Mzee kwani Takukuru si ipo inayopambana na rushwa au haujui kazi yake. Unaongelea habari ya rushwa baada ya kushindwa,” amesema Mikael

Advertisement