Mwalimu mbaroni tuhuma rushwa ya ngono ili ampe amani mwanafunzi

Thursday January 9 2020

 

By Mussa Juma, Mwananchi [email protected]

Arusha. Taasisi za ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Arusha nchini Tanzania, inamshikilia mwalimu wa shule ya Sekondari, Embarway wilaya ya Ngorongoro, William Mollel kwa tuhuma za kumuomba rushwa ya ngono mwanafunzi wake.

Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Arusha, Frida Wikesi akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Januari 9, 2020 amesema mwalimu huyo anayefundisha somo la uchumi, kidato cha tano na sita amekuwa akimnyanyasa mwanafunzi huyo akiwa shuleni na ndipo akamweleza ili awe na amani, wakifunga shule washiriki kimwili.

Wikesi amesema baada ya maombi hayo ya rushwa ya ngono, mwanafunzi alikwenda kutoa taarifa Takukuru Januari 8, 2020 ambapo waliandaa mtengo na kufanikiwa kumkamata mwalimu huyo, akiwa chumbani na mwanafunzi akitaka ngono.

Mwalimu huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani, kujibu tuhuma za rushwa ya ngono kwa mwanafunzi.

 

Advertisement