Precision yapata mkurugenzi mpya

Tuesday November 5 2019

 

By Mwandishi Wetu, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam.  Baada ya miezi saba ya kukaimu, bodi ya wakurugenzi wa Shirika la Ndege la Precision limemteua Patrick Mwanri (44) kuwa mkurugenzi mtendaji kuanzia Novemba Mosi.

Taarifa iliyotolewa na mwenyekiti wa shirika hilo, Michael Shirima  imesema Mwanri anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Sauda Rajab ambay eutumishi wake uliisha mapena Machi.

“Bodi ina imani na Mwanri ndiyo maana imethibitisha uteuzi wake, tunategemea atatumia ipasavyo uzoefu wake wa masuala ya anga kushamirisha biashara na kufikia malengo ya shirika,” amesema Shirima.

Taarifa ya mwenyekiti huyo imetolewa leo, Novemba 5, 2019 kuujuza umma juu ya mabadiliko hayo akiahidi huduma bora kwa wateja wao.

 

 

Advertisement

Advertisement