VIDEO: RC Moro azungumzia hali za majeruhi ajali ya lori la mafuta

Monday August 12 2019Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Stephen Kebwe 

Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Stephen Kebwe  

By Lilian Lucas, Mwananchi [email protected]

Morogoro. Majeruhi wa ajali ya moto iliyotokea juzi Jumamosi Agosti 10,2019 mkoani Morogoro nchini Tanzania inaendelea vyema huku miili 60 imezikwa jana Jumapili katika makaburi ya kola Mkoa huo.

Hadi jana jioni, vifo vilivyokuwa vimeripotiwa kutokana na ajali hiyo ni 72 na majeruhi zaidi ya 59 ambapo baadhi wamelazwa Hospitali ya Rufaa ya Morogoro na wengine wakihamishiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kwa matibabu zaidi,

Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Stephen Kebwe akizungumza na wanahabari leo Jumatatu Agosti 12,2019 akiwa katika eneo la chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya rufaa mkoa wa Morogoro.

Dk Kebwe amesema majeruhi 16 waliopo hospitali ya rufaa mkoa wa Morogoro na majeruhi 43 waliopo hospitali ya taifa ya Muhimbili inaendelea vizuri.

Amesema mpaka leo Jumatatu asubuhi familia mbili zimejitokeza kuzika marehemu wao wenyewe huku mwili mmoja ukipelekwa Sengerema mkoani Mwanza na Songea Mkoa wa Ruvuma.

Amesema mwili mmoja utazikwa asubuhi hii makaburi ya kola  na mwingine utazikwa jioni.

Advertisement

"Niwaeleze tu kuwa hadi sasa hali inaendelea kutulia kwani ndugu wanaendelea kujitokeza," amesema.

Dk Kebwe amesema majeruhi 59 wanaendelea kutibiwa vyema katika hospitali za Muhimbili na Morogoro.

Aidha amesema hakuna kifo kilichoendelea kutokwa tangu jana.

Endelea  kufuatilia Mwananchi kwa habari zaidi

Advertisement