Rais Poland aambukizwa corona

Rais wa Poland, Andrzej Duda

Muktasari:

Duda amegundulika kuwa na maambukizi siku chache baada ya kuhudhuria kikao cha uwekezaji na kukutana na rais wa Bulgaria ambaye baadaye alijiweka karantini.

Warsaw, Poland (AFP). Rais wa Poland, Andrzej Duda amegundulika kuwa na maambukizi ya virusi vya corona, msaidizi wake amesema leo Jumamosi, huku nchi hiyo ikikabiliwa na ongezeko kubwa la maambukizi.

"Mabibi na mwabwana, kama ilivyoshauriwa (kupima) Rais @AndrzejDuda amekutwa na virusi vya corona baada ya kufanyiwa upimaji. Vipimo vimeonyesha kuwa ana maambukizi. Rais yuko katika hali nzuri," alisema Blazej Spychalski, katika katika ofisi ya rais katika akaunti ya Twitter.

Wakati haikueleweka Duda aliambukizwa lini, rais huyo alihudhuria jukwaa la uwekezaji mjini Tallinn Jumatatu ambako alikutana na rais wa Rumen Radev ambaye baadaye aliingia katika karantini.

Poland iliingia katika hatua kubwa ya kudhibiti maambukizi Jumamosi, ikiwa ni pamoja na kufunga shule na hoteli kwa kiwango fulani.

Hatua hiyo imekuja wakati nchi hiyo yenye watu milioni 38 ikiweka rekodi ya maambukizi mapya13,632 ndani ya saa 24.

Wananchi wa Poland wametakiwa kufanya kazi nje ya ofisi kama wanaweza na shule za msingi kufungwa isipokuwa daraja la kwanza hadi la tatu.