Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Walimu watakaojitolea kufundisha miezi saba wilayani Temeke kuajiriwa

Mkurugenzi wa manispaa ya Temeke, Lusubilo Mwakabibi akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam

Muktasari:

  • Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam  imesema walimu wa sayansi watakaojitolea kufundisha wanafunzi kuanzia Januari hadi Julai, 2020  watapewa kipaumbele  wakati wa kuajiri.

Dar es Salaam. Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam  imesema walimu wa sayansi watakaojitolea kufundisha wanafunzi kuanzia Januari hadi Julai, 2020  watapewa kipaumbele  wakati wa kuajiri.

Mkurugenzi wa manispaa hiyo, Lusubilo Mwakabibi alieleza hayo jana Jumatatu Januari 27, 2020 wakati akitangaza fursa mpya ya ajira ya walimu 155 wa masomo ya sayansi ili kukabiliana na uhaba wa walimu katika manispaa hiyo.

Mwakabibi amesema Julai Mosi, 2020 wataajiri walimu wapya wa sekta wa sayansi ambao mishahara yao itatokana na makusanyo ya manispaa hiyo.

Amesema wanaohitajika ni walimu wa kemia, fizikia, hesabu, baiolojia, kwamba wanatakiwa walimu 400 ila kwa sasa wanaanza na 155.

Kwa mujibu wa Mwakabibi, katika matokeo ya kidato cha nne mwaka 2019 manispaa ya Temeke imejitahidi kufanya vizuri katika masomo ya sanyasi, lakini walichokibaini ni uhaba wa walimu wa sayansi, si miundombinu.

“Manispaa ya Temeke ina shule za sekondari takribani 31 kila moja itapata walimu watano. Julai Mosi, 2020 tutaajiri kwa mikataba ya muda, na  ili mwalimu  apate mkataba mwingine itategemea na ufanisi wake, hasa matokeo ya wanafunzi,” amesema Mwakabibi.

 Amesisitiza kuwa walimu watakaojitolea kufundisha kuanzia sasa watapewa kipaumbele cha ajira tofauti na watakaofanya usaili baadaye.

Amesema sifa ni mwalimu kuwa na shahada.