Ziara za Majaliwa zilivyoondoa vigogo wa wilaya

Wednesday September 18 2019

 

By Mwandishi Wetu, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa hateuwi wakuu wa mikoa, wilaya,wakurugenzi wala makatibu wa ngazi hizo lakini sasa anaweza kuwa mwiba mkali kwa wateule hao wa Rais John Magufuli.

Ziara zake zimekuwa chungu kwa watumishi wa umma wa ngazi hizo kwani kila anapomaliza baadhi hujikuta wamechukuliwa hatua na Rais Magufuli kutokana na kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo, au kuingiza ubinafsi na kuzorotesha maendeleo.

Mwananchi linakuorodhoshea baadhi ya watumishi waliokumbwa na hali hiyo baada ya Majaliwa kumaliza ziara katika maeneo yao.

Januari 8, 2018 Waziri Mkuu akiwa katika ziara yake Nyasa mkoani Ruvu-ma alimwambia mkuu wa wilaya hiyo, Isabella Chilunda na mkurugenzi wake wa halmashauri, Dk Oscar Mbyuzi kuondoa tofauti zao kwa kuwa zinaathiri watendaji walio chini na kuwaumiza wananchi. April 9, 2019 Rais Magufu-li alitengua uteuzi wa mkurugenzi huyo baada ya kufanya ziara wilayani hapoDk Oscar Mbyuzi
Dk Oscar Mbyuzi

Januari 22, 2018 Majaliwa akiwa ziarani Butiama mkoani Mara aliagiza kuchunguzwa kwa watumishi wa halmashauri ya mji huo, akiwamo mkurugenzi mtendaji, Solomon Ngiliule kutokana na tuhuma za matumizi ya fedha za maendeleo kwa shughuli nyingine. Januari 23, 2018, Rais Magufuli alitengua uteuzi wa Solomon kutokana na kushindwa kutimiza majukumu yake.

Advertisement

 Julai 16, 2018 Majaliwa akiwa wilayani Kahama, Shin-yanga alieleza kutokuwepo kwa maele-wano kati ya mkuu wa wilaya, Fadhil Nkulru na viongozi wenzake, akiwemo mkurugenzi mtendaji (Ded). Saa chache baadae Rais Magufuli alitengua uteuzi wa Fadhil.

Fadhil Nkulru akisalimiana na Waziri mkuu wa
Fadhil Nkulru akisalimiana na Waziri mkuu wa Tanzania Kasimu Majaliwa katika moja ya ziara yake

 Sept 16, 2019 Akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Morogoro, Majaliwa alichukizwa na mgongano uliopo kati ya mkuu wa wilaya ya Malinyi, Majura Kasika na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, Mussa Mnyeti. Watendaji hao wanadaiwa kugombana na wakati mwingine chanzo ni miradi. Jana asubuhi Rais Magufuli alitangaza kutengua uteuzi wa watumishi hao.

Majura Kasika akisalimiana na Waziri mkuu wa
Majura Kasika akisalimiana na Waziri mkuu wa Tanzania Kasimu Majaliwa katika moja ya ziara yake

Idadi ya watumishi 15 ambao Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa aliagiza wasimamishwe kazi; Saba ni wa Halmashauri ya Kilombelo na Mji Ifaraka wakituhumiwa kwa ubadhilifu wa Sh1.3 bilioni alizoagiza wazirudishe, na nane ni wa Halmashauri ya Ulanga wanaotuhumiwa kwa ubadhilifu wa zaidi ya Sh3 bilioni. Majaliwa yupo mkoani Morogoro anaendelea na ziara ya kikazi ya siku tano.

Advertisement