Alikiba abeba tuzo tano TMA
Muktasari:
- Ali Kiba jana amerudisha heshima yake aliyoiachia mwaka 2015, baada ya kushinda tuzo tano za Muziki Tanzania (TMA).
Dar es Salaam. Ali Kiba jana amerudisha heshima yake aliyoiachia mwaka 2015, baada ya kushinda tuzo tano za Muziki Tanzania (TMA).
Tuzo hizo zilitoleaa jana Jumamosi Aprili 2,2022 jijini Dar es Salaam ni tuzo za kwanza kusimamiwa na Serikali.
Kiba ameongoza kupata tuzo nyingi kuliko wasanii wengine wa bongo fleva.
Kiba amepata tuzo katika kipengele cha Albamu Bora ya Mwaka, Mtunzi Bora wa Melody, Video Bora ya Wimbo kupitia wimbo wake wa ‘Salute’, msanii Bora wa Kiume Afrika Mashariki na msanii Bora wa Kiume chaguo la watu.
Hatua hiyo inamfanya Ali Kiba kurudia historia yake aliyoiweka mwaka 2015 katika Tuzo za Kilimanjaro ambapo pia alishinda tuzo tano.
Baadhi ya watu waliohudhuria hafla hiyo akiwemo Emima Lazaro na Francis Abel, wameeleza kuwa Alikiba amestahili ushindi huo kutokana na juhudi zake za muziki.
Kwa upande wao uongozi wa msanii huyo umeeleza kuwa ushindi huo ameutoa kwa watanzania wote kama zawadi kwao kwa namna wanavyomsapoti katika kazi yake ya muziki.