Bob Marley alivyompatia maokoto rafiki yake
Miongoni mwa nyimbo kubwa za Bob Marley ni pamoja na hii ya ‘No Woman No Cry’ iliyotoka mwaka 1974 ikiwa moja ya ngoma zinazopatikana kwenye albamu yake ya Natty Dread.
Kabla ya Bob Marley kuuachia, alimuweka rafiki yake Vincent Ford kama mwandishi mwenza wa wimbo huo ambapo kwa kipindi hicho Ford alikuwa anajihusisha na biashara ya kuuza supu mji wa Trench sehemu aliyokulia Bob Maley huko nchini Jamaica.
Bob Marley alifanya uamuzi huo ili Ford awe sehemu ya watu wanaopokea mirabaha (mauzo) ya kazi hiyo ili aendeleze biashara hiyo ya supu ambayo ilikuwa inasaidia kwenye mitaa aliyokulia mwanamuziki huyo, na kusadia biashara hiyo kuendelea kwa zaidi ya miaka 30.
Uamuzi huo ulipelekea Bob kuingia mzozo wa kimkataba na kampuni ya K Man Music iliyokuwa ikisimamia uchapishaji wa kazi zake kwa kumuandika Ford lakini hawakufanikiwa kwani tayari Ford alikuwa akitambulika kama mwandishi mwenza wa kazi hiyo.