Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jiongeze: Kuwa Jide au Mona ni ushujaa

Muktasari:

  • Also men do it. sijui ndiyo kuwaiga wenzetu wa kule Congo? Inakera wengine vidole kama mahindi ya kuchoma.

Dar es Salaam. Huenda Mungu akawa na wapinzani wengi zaidi, maana kujichubua ni kupinga uumbaji wake, kwamba wameumbwa visivyo! hii leo siyo wadada tu wanaojichubua.

Also men do it. sijui ndiyo kuwaiga wenzetu wa kule Congo? Inakera wengine vidole kama mahindi ya kuchoma.

 Wazungu a.k.a mabeberu wameshajua udhaifu wetu watu weusi. Kwenye mitandao ya kijamii kuna utundu wameweka wa kusafisha picha ya mtu mweusi kuonekana mweupe, au mwenye ngozi nyororo lakini hakuna utundu wa kumfanya mweupe awe mweusi.

 Hivi juzi kuna mchezo flani wa kipimbi tu ukiitwa "Ten Years Challenge", yaani mtu anaweka picha yake ya miaka 10 nyuma na ya sasa.

Kisha anasindikiza na maneno ya #TenYears Challenge. Madem wengi wa mjini waliupuuza maana haukuwa rafiki na ngozi zao za kale.

 Kwa mfano Instagram unaweza kudhani kila msichana ni mweupe na hana chunusi. Wanafurahia kujidanganya, ni kama kulewa ili upunguze mawazo wakati mawazo hayaishi.

Msichana wa kizazi hiki kuwa Monalisa au LadyJaydee, yaani ngozi kubaki vilevile ni ushujaa.