Jiongeze: Majizzo yupo sahihi, lakini muda unamkataa
Muktasari:
- Ila komenti zinamkataa, Gen Z wameshikilia bomba. Ukimsikiliza kwa sikio la kiroho, kuna ‘toni’ ya kooni ya uchungu wa mzazi kwa muziki na wanamuziki.
Dar es Salaam. Umemsikiliza Big Boss Majizzo? Tumbo lake la uzazi wa muziki limemcheza. Ameshindwa kukaa kimya, kajitokeza kuomba radhi kwa niaba ya masela.
Ila komenti zinamkataa, Gen Z wameshikilia bomba. Ukimsikiliza kwa sikio la kiroho, kuna ‘toni’ ya kooni ya uchungu wa mzazi kwa muziki na wanamuziki.
Mwendo wa sanaa na wasanii siyo mzuri kwa sasa, kuna kiza kinene. Bahati mbaya wakati unamkataa Jizzo. Amechelewa kunena yale aliyonena juzi kati.
Alichopaswa kukisema miaka mingi iliyopita, kakisema leo bomu likiwa tayari kulipuka malaika wamegoma. Tulisema na kuandika sana kwenye hili.
Kwamba zinaua vipaji na sanaa, tulionya wasanii kutumika kisiasa ambayo watu wanaokuja na kuondoka. Hatukueleweka na pengine tuliitwa wenye wivu.
Kutumika siyo tatizo, tatizo ni unatumikaje? Kuna baadhi yao walitumika au kujitumikisha vibaya. Kwa lugha au matendo yasiyofaa, hawa ndiyo chanzo cha fyoko fyoko zote.
Busara za Majizzo ni njema na sahihi, lakini muda huu hazina nguvu sana. Ni kama kulishana upepo, watu hawaelewi kwa sasa zaidi ya walichoamua. Tuwape muda, kuna wakati wimbi hutulia