Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jux alivyomfungulia dunia Mimi Mars

Muktasari:

  • Ameshinda tuzo za muziki Tanzania (TMA) na East Africa Arts & Entertainment Awards (EAEA), huku akitoa albamu mbili, The Love Album (2019) na King of Hearts (2022) ambazo zimeonyesha ukubwa wa kipaji chake. Huyu ndiye Jux;.

Dar es Salaam. Kwa miaka zaidi ya 10 Jux amekuwa na mwendelezo wa kufanya vizuri katika Bongofleva akitamba hasa katika miondoko ya RnB na Amapiano hadi kuijenga chapa na himaya yake kama staa mkubwa wa muziki Afrika Mashariki.

Ameshinda tuzo za muziki Tanzania (TMA) na East Africa Arts & Entertainment Awards (EAEA), huku akitoa albamu mbili, The Love Album (2019) na King of Hearts (2022) ambazo zimeonyesha ukubwa wa kipaji chake. Huyu ndiye Jux;.

1. Kuna nyimbo za Jux ameandikiwa na wasanii wenzake, nyimbo hizo ni Sisikii (2015) umeandikwa na Mabeste, Unaniweza (2020) umeandikwa na Marioo, na Enjoy (2023) umeandikwa na Lody Music ambaye pia kaandika wimbo wa Nandy, Napona (2022).

2. Jux ni msanii wa 12 nchini Tanzania kufikisha wafuasi (subscribers) zaidi ya milioni 1 YouTube akiwa ni mmoja ya wasanii wachache waliofika namba hizo ndani ya muda mfupi akiwa amejiunga na mtandao huo hapo Oktoba 5, 2018.

Diamond Platnumz ndiye msanii wa kwanza kufanya hivyo kisha akafuata Harmonize, Rayvanny, Mbosso, Zuchu, Alikiba, Lava Lava, Nandy, Marioo, Aslay na Rose Muhando.

3. Wimbo wa Jux, Sina Neno (2022) ilitoka baada ya aliyekuwa mpenzi wake, Vanessa Mdee kubeba ujauzito, hiyo ni sawa na Rayvanny ambaye ametoa wimbo wake, Hongera (2024) kufuatia aliyekuwa mpenzi wake, Paula naye kubeba ujauzito!.

4. Licha ya kufanya kazi na watayarishaji muziki mbalimbali ambao wametengeneza nyimbo zake nyingi kali, bado Manecky wa AM Records anabaki kuwa Prodyuza bora wa muda wote kwa Jux maana ndiye alitengeneza nyimbo zilizomtambulisha.

5. Video ya wimbo wa Jux, Enjoy (2023) akimshirikisha Diamond Platnumz ndio iliyotazamwa zaidi YouTube Afrika Mashariki kwa mwaka uliopita ambapo ilipata 'views' zaidi ya milioni 42 ndani ya miezi 10 tangu kuachiwa kwake.

Tangu ameanza kuvuma kimuziki akiwa na kundi la Wakacha, huo ndio wimbo wa kwanza wa Jux kupata namba kubwa YoTube, ukifuatiwa na 'Sugua' kutoka katika albamu yake, The Love Album (2019), huku akimpa tena shavu Diamond.

6. Wakati wanaenda kushuti video ya wimbo wao, Sumaku (2019), Jux na Vanessa tayari walikuwa wameshaachana ili iliwabidi kuweka tofauti zao za kimahusiano pembeni na kufanya kazi hiyo ambayo ndio mwisho kutoka kwao. 

7. Jux ana shahada ya Computer Science aliyoipata katika chuo cha Guangdong nchini China, wasanii wengine Bongo wenye taalamu sawa na hiyo ni Roma (UDSM), Nahreel (Punjab College, India) na Nikki Mbishi (MUST).

8. Hadi sasa ni warembo wawili ambao Jux amewahi kuwa na uhusiano nao na kuwatumia katika video za nyimbo zake, kuna Vanessa aliyetokea katika video ya wimbo, Sisikii (2015), na Nayika kutokea Bangkok, Thailand katika video ya wimbo, Unaniweza (2020).

9. Kipindi Mimi Mars hajatoka kimuziki, Jux alimshawishi Quick Rocka kumshirikisha mrembo huyo katika wimbo wake, Down (2017) ambao ulitengenezwa katika studio yake ya Switch Music Group (SMG).

Licha ya Quick Rocka kutowahi kumsikia akiimba popote pale alikubali kutokana anajua Jux hawezi kumpendekeza kwake mtu asiyekuwa na uwezo. Wimbo ukatoka na ukawa mwanzo wa Mimi Mars kutambulika kabla ya kuja kusainiwa Mdee Music.

10. Jux ni msanii wa kwanza wa Bongofleva kutoka nje ya WCB Wasafi kumshirikisha Zuchu katika wimbo wake. Zuchu amesikika katika wimbo wa Jux 'Nidhibiti' kutoka katika albamu yake ya pili, King of Hearts (2022).

Kabla ya hapo, Zuchu alikuwa ameshirikiana na wasanii wa WCB Wasafi pekee ila Jux akawa wa kwanza kisha akafuata Darassa ambaye amempa shavu Zuchu katika wimbo wake mpya, Romeo (2024) unaofanya vizuri kwa sasa.