Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kazi ya S2kizzy 2025 ni ya kibabe zaidi

Asilimia kubwa ya nyimbo za Bongofleva zilizofanya vizuri mwaka huu na kukaa katika chati kwa muda mrefu, zimepita katika mikono ya S2kizzy ambaye alianza kazi hiyo tangu alipomaliza kidato cha nne. 

Mtayarishaji muziki Bongo kutokea studio za Pluto Republic, S2kizzy a.k.a Zombie anaenda kuufunga mwaka kwa furaha zaidi kama sio kibabe kufuatia mafanikio makubwa ya kazi nyingi alizotayarisha 2025. 

Asilimia kubwa ya nyimbo za Bongofleva zilizofanya vizuri mwaka huu na kukaa katika chati kwa muda mrefu, zimepita katika mikono ya S2kizzy ambaye alianza kazi hiyo tangu alipomaliza kidato cha nne. 

Je, wajua wimbo wa Bongofleva uliosikilizwa zaidi katika mtandao wa Spotify kwa mwaka huu umetayarishwa na S2kizzy?, ndiyo ni yeye, nao ni Pawa (2025) wake Mbosso, mwanachama wa zamani wa Yamoto Band.

Ni wimbo unaopatikana katika Extended Playlist (EP) ya pili yake Mbosso, Room Number 3 (2025) ambayo pia S2kizzy amehusika kutengeneza nyimbo nyingine huko kama Aviola, Merijaah na Tena.

Hivyo katika EP hiyo yenye nyimbo saba ikiwa ni ya kwanza chini ya Khan Music, S2kizzy ndiye mtayarishaji aliyeingiza nyimbo nyingi zaidi katika mradi huo ambazo ni nne kwa ujumla.

Room Number 3 EP (2025) ni mradi uliotoa matokeo makubwa zaidi na ya haraka, mathalani video ya muziki iliyotazamwa zaidi YouTube Bongo kwa mwaka huu inatokea hapo.

Nayo ni ya wimbo 'Pawa' ambao Skizzy kauhusika pia, video hiyo iliyosimamiwa na Director Folex imeshatazamwa katika mtandao huo zaidi ya mara milioni 53 ikiwa ni miezi sita tangu kuachiwa kwake.

Tangu akiwa Yamoto Band, WCB Wasafi hadi sasa Khan Music, huu ndio wimbo wa Mbosso uliofanikiwa kuwa namba moja YouTube na Spotify ndani ya mwaka ulioachiwa.

Na kama unadhani S2kizzy kabatisha katika ngoma hiyo (Pawa) kwa vile tayari Mbosso ana nguvu ya ushawishi katika tasnia, utakuwa umemkosea tena sana.

Je, wajua katika orodha ya nyimbo za Bongofleva ambazo video zake zimefanya vizuri zaidi YouTube kwa huu sita kati ya hizo S2kizzy ndiye amezitayarisha?.

Ndiyo, ukiacha 'Pawa' ulioshika namba moja, S2kizzy ana nyimbo nyingine tano ambazo zimefanya vizuri na kuingia 10 bora ya zile video za muziki zilizotazamwa zaidi katika mtandao huo kwa mwaka huu.

Nyimbo hizo ni 'Tete' wake Marioo ambao video yake imetazamwa YouTube zaidi ya mara milioni 37 ndani ya miezi minane na kushika nafasi ya tatu katika 10 bora ya 2025.

Nyingine ni 'Me Too' wake Abigail Chams, huu video yake imeshika namba tano ikiwa imetazamwa mara milioni 28. Pia kuna 'Salama' wake Barnaba ambao umetazamwa mara milioni 26 kwa miezi sita na kushika nafasi ya sita.

Vilevile kuna 'Amanda' wake Zuchu ukitazamwa mara milioni 14 huku ukikamata nafasi tisa, kisha kuna 'Katam' wake Diamond Platnumz, huu umekamata nafasi ya 10 baada ya kutazamwa mara milioni 14.

Hiyo ndio kazi aliyoifanya S2kizzy kwa mwaka huu, na mbali ya nyimbo hizo kufanya vizuri YouTube, pia zimekuwa na matokeo chanya zaidi kichapa na kibiashara kwa baadhi ya wasanii.

Mathalani wimbo wa Abigail Chams, Me Too (2025) kufanya kwake vizuri kulipelekea staa huyo kuchaguliwa kuwania tuzo za BET huko Marekani kwa mara ya kwanza.

Mbali na hilo, pia Abigail akaweka rekodi kama mwanamuziki wa kwanza wa kike Afrika Mashariki kuwania tuzo hizo, na watatu kwa ujumla kwa hapa Tanzania baada ya Diamond na Rayvanny. 

Pia wimbo wa Zuchu, Amanda (2025) ulikuwa na mchango kwa mwimbaji huyo kupata nafasi ya kutumbuiza katika fainali ya CHAN 2024 iliyofanyika Kenya, na huu ndio ulikuwa wimbo wake wa kwanza jukwaani.

Na huyo ndiye S2kizzy ambaye alianza kupata umaarufu baada ya kutengeneza ngoma ya Country Wizzy, Aah Wapi (2016). Mdundo wake uliwavutia wengi hasa DJ's wa kwenye redio walioutumia mara kwa mara.

Ndipo akaja kukutana na Quick Rocka ambaye alimpa nafasi katika studio yake, Switch Records na hapo ndipo S2kizzy akafahamiana na wasanii mbalimbali wakubwa wa Bongofleva.

Wakati anajiunga Switch, watayarishaji wawili walikuwa wameondoka katika studio hiyo, nao ni Nahreel aliyeenda kufungua The Industry, na Luffah aliyehamia studio za Wanene.

Hata hivyo, mwisho siku naye S2kizzy aliondoka na kufungua studio yake, Pluto Republic ambayo sasa imekuwa umaarufu ikifanya kazi kwa ukaribu na mastaa kama Diamond, Zuchu, Jux na Nandy.

Wengine ni Marioo Rayvanny, Lulu Diva, Harmonize, Country Wizzy, Joh Makini, Mbosso, G Nako, Billnass, Ommy Dimpoz, D Voice, Young Lunya, Abigail Chams, Moni Centrozone, Weusi, Barnaba n.k.