Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Khadija Kopa atoa kauli ndoa ya Diamond, Zuchu kufungwa kisiri

Muktasari:

  • Khadija Kopa amevunja ukimya baada ya video kusambaa mtandaoni ikimuonyesha mwanaye Zuchu akifungishwa ndoa na Diamond.

Dar es Salaam. Malkia wa Mipasho nchini Khadija Kopa ambaye ni mama mzazi wa msanii Zuchu ametoa kauli kuhusu ndoa ya mwanaye Zuhura Othman Soud na staa wa Bongo Fleva, Nassib Abdulmaarufu Diamond.

Diamond na Zuchu wanadaiwa kuoana kwa siri baada ya kusambaa video ikiwaonyesha wawili hao wakifungishwa ndoa.

Akizungumza na Mwananchi leo Juni 2, 202 amesema kuwa taarifa ya binti yake kuolewa hata yeye anaiona kwenye mitandao ya kijamii kama watu wengine.

"Mngewauliza wenyewe mimi siyo niliyeolewa. Waulizeni wenyewe waliokwenda kuoana mimi sijui. Sijapokea mahari kawaida anapokea aliyeolewa sisi waislamu mahari ni ya mtoto wa kike siyo yangu," amesema.

Hata hivyo, alipoulizwa kuhusiana na video inayomuonesha akiwa kwenye gari akishangilia ndoa ya binti yake mama huyo alijibu, 

"Mimi nimeona kwenye mitandao sijui. Sasa nishaambiwa kwamba kaolewa kwanini nisisherehekehe. Lakini waulizeni wenyewe,"amesema.

Utakumbuka kuwa jana Juni 1,2025 Diamond kwenye ukurasa wake wa Instagram alichapisha picha na video zikionesha akifunga  ndoa akizisindikiza na ujumbe uliosomeka.

"Miongoni mwa vitu ambavyo nimejifunza ni ukomavu wa kukaa kimya. Ukomavu huu unataka uvumilivu wa hali ya juu, inataka uwe na moyo wa subra na hasa kukaza roho pindi mtu au watu wanapokuwa wanakupakazia ubaya fulani kwenye jamii halafu wewe una ukweli wake lakini unatakiwa ukae tu kimya usijibu ilhali ukweli unao ndani.

"Kwakweli si jambo jepesi linataka ustahimilivu wa hali ya juu sana na siwezi kusema eti nauweza sana, lakini namshukuru mwenyezi Mungu amenijaalia hekima hiyo kwa kiwango chake na nimekuwa nikiishi hivyo kwa muda mrefu kukaa kimya pindi yoyote akijaribu kusema lolote zaidi yangu na ndio maana hata interview nimekua naepuka kufanya siku hizi.

"Japo si jambo jepesi lakini faida yake nimeiona na ni kubwa maana vita yako inakuwa unapambaniwa na mwenyezi Mungu na inakufanya uwe mshindi kila siku. Anyways najua kila mmoja wenu ana picha tofauti kabisa kuhusu Diamond Platnumz na kuoa. lla tu nataka leo niwaambie kuwa huyu Diamond Platnumz alishawahi kuoa na kuna siku nitawaambia ikawaje,"amesema.

Licha ya ujumbe huo katika moja ya video aliyochapisha alisikika akitamka maneno haya, "Nimekubali kumuoa Zuhura Othaman kwa mahari yake tuliyokubaliana,"anasikika Diamond kwenye video hiyo.

Licha ya taarifa hiyo kusambaa mtandaoni Mei 28, 2025 wakati sherehe ya harusi ya msanii Juma Mkambala na mkewe Prisca, Zuchu katika mahojiano yake na Wasafi TV aliuzwa kuhusu kama wana mpango wa kuoana na Diamond hivi karibuni na akajibu haoni huo mpango.