Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kumbe ishu ya Mbosso kudondoka baharini ipo hivi 

Muktasari:

  • Mapema jana Mbosso alichapisha video ikionesha ameteleza na kuangukia baharini tukio ambalo liliwaachia maswali mashabiki. Kwa sasa inaelezwa kuwa msanii huyo ni mzima wa afya na hajapata tatizo lolote.

Dar es Salaam. Baada ya kuzuka kwa taharuki kuhusiana na tukio alilokumbana nalo Mwanamuziki wa Bongo Fleva nchini, Mbosso la kuangua baharini wakati wa kushuti. Hatimaye amelitolea ufafanuzi kuhusu tukio hilo.

Mapema jana Mbosso alichapisha video ikionesha ameteleza na kuangukia baharini tukio ambalo liliwaachia maswali mashabiki. Kwa sasa inaelezwa kuwa msanii huyo ni mzima wa afya na hajapata tatizo lolote.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameshare video nyingine huku akiandika kuwa “Tunaanguka, Tunainuka, Tunajaribu tena hadi tufanikiwe, inawezekana.” 

Hata hivyo msanii huyo ameweka wazi kuwa tukio hilo ni maandalizi ya filamu yake ambayo hakuitolea maelezo kamili kuwa ni filamu ya aina gani.  

“Sijaumia popote, parefu pale sema waliniwahi nilikuwa nashoot filamu fulani hivi,” amesema Mbosso.

Mbali na tukio hilo Mbosso amekiwasha kwenye kilele cha tamasha la klabu ya Simba 'Simba Day' tukio ambalo limefanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
 
"Najua watu wengi wanafahamu mimi ni msanii wa muziki wa kizazi kipya, nimekuwa nikitumia talanta yangu katika sanaa ya muziki, hivyo nimeamua kutoa 'surprise' kwenye tukio la Simba Day kwa ajili ya mashabiki wa Simba.

“Kutunga wimbo maalumu wa Simba ama kutumia nyimbo zangu za Bongofleva, hii ni siri yangu ila kikubwa niwaombe mashabiki wa Simba Septemba 10 wafike kwa wingi kwa ajili ya kushuhudia burudani nitakayoitoa," alisema Mbosso.

Kwa sasa Mbosso anatamba na albamu yake ya Room Namba 3 yenye nyimbo Pawa, Nusu saa, Aviola, Tena, Siko Single, Athuman, Merijah.