Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kwanini mke wa Bieber alificha ujauzito?

Muktasari:

Mnamo Mei 2024, Bieber (27), na Hailey (27), kupitia mitandao ya kijamii walitangaza kuwa wanatarajia kupata mtoto wao wa kwanza tangu wafunge ndoa ya kiserikali huko New York, Marekani Septemba 2018.

Marekani, Hatimaye mke wa mwimbaji wa Pop kutoka nchini Canada, Justin Bieber, Hailey amefunguka sababu ya kuficha ujauzito wake mbele ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kwa miezi sita.

Mnamo Mei 2024, Bieber (27), na Hailey (27), kupitia mitandao ya kijamii walitangaza kuwa wanatarajia kupata mtoto wao wa kwanza tangu wafunge ndoa ya kiserikali huko New York, Marekani Septemba 2018.

Wawili hao kwa mara ya kwanza walikutana Novemba 2009 katika kipidi cha Today Show ila Machi 2016 ndipo Bieber alithibitisha uhusiano wao na kumtaja Hailey kama mtu anayempenda sana na wamekuwa wakitumia muda mwingi pamoja.

Katika mahojiano na W Magazine yaliyochapishwa wiki hii, Hailey amesema tumbo lake lilikuwa dogo sana kwa muda mrefu hadi alipofikisha miezi sita ndipo angalau likaonekana kama lina kiumbe ndani yake.

“Sikuwa na tumbo kubwa kwa kweli ni hadi pale nilipokuwa na ujauzito wa miezi sita ndipo nikatangaza. Nilikuwa naweza kuvaa koti kubwa na vitu vingine,” alisema Hailey.

“Hata hivyo, nilihisi kama nilikuwa nikificha siri hii kubwa na kwa kweli sikujisikia vizuri. Nilitaka uhuru wa kutoka nje na kuishi maisha yangu ya kawaida.”

Lakini mtangazaji huyo wa zamani wa kipindi cha Drop the Mic alisema ingawa hataki kujitia hofu ila mtandaoni siyo sehemu salama sana kwa mjamzito na angeweza kufanya jambo hilo siri hadi atakapojifungua.

“Mtandao ni mahali pa kutisha kwa mwanamke mjamzito. Unaona hadithi nyingi, za kushikwa na kiwewe na uzoefu wa kutisha na ninajua kuwa hilo ni kweli kabisa lakini sitaki kujitia hofu,” alisema Hailey.

Hailey ambaye Septemba 2023 wakati wanatimiza miaka mitano ya ndoa yao alikanusha madai ya kuwa mjamzito, amesema kipindi cha mwanzo cha ujauzito wake kiliambatana na hisia nyingi mseto.

“Mwanzoni kipindi cha ujauzito, nilikuwa na hisia nyingi sana, nilimwambia mama, ‘Ninampenda huyu mtu (Bieber) sana, ninawezaje kumleta mtu mwingine duniani katika hali hii?” alisema Hailey.

Hata hivyo, Hailey alisema kwa sasa hayuko karibu sana na familia yake kitu kinachomfanya kuwa huru sana. Anapenda kuishi maisha ya faragha na kuijenga familia yake mwenyewe.

Ikumbukwe mwaka mmoja baada ya Bieber na Hailey kufunga ndoa huko South Carolina, walifanya harusi yao kubwa iliyohudhuriwa na familia, ndugu na marafiki wao zaidi ya 150 katika hoteli ya Montage Palmetto Bluff.

“Alikuwa mtu wa kwanza kuwa na hisia naye za kweli, wakati mambo yalikwenda mrama, nilisema haijalishi itakuwaje ila bado ni mtu ambaye nilimpenda maisha yangu yote, siku zote alikuwa akishikilia nafasi maalum katika moyo wangu,” alisema Hailey Februari 2020.