Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Luiza Mbutu: Msitegemee nyota yangu kuzima

MBUTU Pict

Muktasari:

  • Luiza Mbutu ambaye ni mtunzi wa wimbo maarufu wa ‘Kuolewa’ wa Twanga Pepeta amesema anamshukuru Mungu kwa kumjalia nyota hiyo ambayo inawezekana kuna watu wanatamani izimike wakati wowote, jambo ambalo haliwezekani leo wala kesho na kwa kuwa alitoka nayo tumboni kwa mama yake.

Dar es Salaam. Nyota wa muziki wa dansi, Luiza Mbutu, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Bendi ya Twanga Pepeta, ameliambia Mwananchi kuwa hata kama akizeeka na kuwa kikongwe, bado nyota yake itaendelea kung’ara siku zote wala haitafifia kwani amezaliwa nayo labda asiwepo duniani.

Luiza Mbutu ambaye ni mtunzi wa wimbo maarufu wa ‘Kuolewa’ wa Twanga Pepeta amesema anamshukuru Mungu kwa kumjalia nyota hiyo ambayo inawezekana kuna watu wanatamani izimike wakati wowote, jambo ambalo haliwezekani leo wala kesho na kwa kuwa alitoka nayo tumboni kwa mama yake.

“Hata kama watu wanasubiri huenda nikizeeka basi jina la Luiza Mbutu litafutika yaani nyota yangu itazimika... kwa hili wasitegemee, nyota yangu itaendelea kung’ara hata nitakapokuwa mzee, nitakuwa ni bibi mwenye mvuto na hata watoto watapenda kusikiliza hadithi zangu,” amesema Luiza.

Kama hufahamu, sifa kubwa ya Luiza Mbutu ni ile ya kutokuhama kwenda bendi nyingine kama wafanyavyo wasanii wengine. Tangu alipoingia Twanga Pepeta, mwaka 1998 akitokea Magoma Moto Sound, hajawahi kuhama hata mara moja.

Aidha, amesema sababu za kutohama ni kutokana na kuwaona waliohama hawajafika popote.