Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Maokoto yafanya Rihanna ajifunge mtandio kiunoni

Muktasari:

  • Rihanna ameonekana kwenye vazi hilo wakati akitoka kuongea na bilionea Mukesh Ambani kwa ajili ya kutumbuiza kwenye tafrija ya sherehe ya harusi ya kijana wake Anant Ambani inayotarajiwa kufanyika wiki hii.

India. Mwanamuziki Rihanna amewashangaza wengi kupitia mitandao ya kijamii baada ya kuonekana akiwa nchini India amejifunga mtandio kiunoni.

Rihanna ameonekana kwenye vazi hilo wakati akitoka kuongea na bilionea Mukesh Ambani kwa ajili ya kutumbuiza kwenye tafrija ya sherehe ya harusi ya kijana wake Anant Ambani inayotarajiwa kufanyika wiki hii.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo vinaeleza kuwa Rihanna amelipwa mpunga mrefu kwa ajili ya kutumbuiza kwenye sherehe hiyo ambapo inadaiwa kuwa amelipwa dola 9 milioni, ambazo ni zaidi ya tsh 22 bilioni.

Hii siyo mara ya kwanza kwa bilionea huyo kuwaita wanamuziki wakubwa kutumbuiza katika sherehe za harusi za watoto wake, mwaka 2018 alimlipa mwanamuziki Beyonce kutumbuiza kwenye harusi ya binti yake Isha Ambani.