Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mastaa watoswa na watazamaji tuzo za filamu

Jacob Steven'JB'

Muktasari:

Mastaa katika fani ya filamu watoswa na watazamaji wao katika kuwania tuzo za  filamu.

Dar es Salaam. Mastaa katika fani ya filamu watoswa na watazamaji wao katika kuwania tuzo za  filamu.

Hivyo ndivyo unavyoweza kusema baada ya maastaa wachache kuteuliwa katika kipengele cha chaguo la watazamaji.

Majina ya wateule watakaowania tuzo hizo yametangazwa leo na Bodi ya Filamu ambapo vipengele 39 vinawaniwa.

Hata hivyo katika kipengele cha chaguo la watazamaji majina ya wasanii maarufu yaliyoonekana hawazidi watano.

Waliotajwa katika kipengele hicho ni Jacob Steven'JB' aliyepenya kupitia tamthilia ya Huba.

Pia yupo Wema Sepetu aliyepenya kupitia filamu ya Malkia, Flora Mvungi kupitia filamu ya Mwali, Hidaya Njaidi kupitia tamthiliya  ya Moyo. 

Ukiacha kwenye kipengele cha chaguo la watazamaji, pia kwenye vipengele vinavyofuatiliwa zaidi ikiwemo msanii bora wa kiume hawajapenya kabisa.

Badala yake waliotajwa katika kipengele hicho  na filamu walizoigiza kwenye mabano ni Gurdin Mwanyika (Vunta N'kuvute), John Kokolo (Wandongwa) na Isaya Lyoba (Nakupenda).

Wengine ni  Nkwabi Ng'wanamala (Kombolela), Saam Nawanda (Merchandizer) na Ayoub Bombwe (Alifu kwa Ujiti).

Wakati kwa wasanii bora wa kike wapo Bi Star, Wema Sepetu ,Irene Paul, Thecla Mjata, Nyota Waziri na Tunu Mbegu.