Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Miaka 10 bila Alikiba kumshirikisha msanii wa kike

Muktasari:

  • Kingine cha kushangaza hata wasanii waliowahi kushirikishwa kwenye nyimbo na Alikiba  ni wakubwa kwake kiumri, mathalani Lady Jaydee na sasa Sabaha Salum ambaye ni mkongwe wa upande taarabu.

Hatimaye wimbo mpya wa Staa wa Bongofleva, Alikiba 'Yalaiti' akimshirikisha Sabaha Salum umehitisha rasmi safari ya zaidi ya miaka 10 kwa mwimbaji huyo wa Kings Music kutomshirikisha msanii wa kike katika nyimbo zake.

Mara ya mwisho kwa Alikiba kumshirikisha mwanamuziki wa kike ilikuwa mwaka 2012 alipotoa wimbo wake 'Single Boy' akiwa na Lady Jaydee, kolabo iliyofanya vizuri ndani na nje ya nchi.

Hata albamu yake ya tatu, 'Only One King' (2021), haikushirikisha msanii wa kike, waliopata nafasi ni Abdukiba, K2ga, Tommy Flavour, Mayorkun, Rudeboy, Nyashinksi, Patoranking, Khaligraph Jones, Blaq Diamond, Sauti Sol na Sarkodie.

Kingine cha kushangaza hata wasanii waliowahi kushirikishwa kwenye nyimbo na Alikiba  ni wakubwa kwake kiumri, mathalani Lady Jaydee na sasa Sabaha Salum ambaye ni mkongwe wa upande taarabu.

Cha kushangaza zaidi katika ukimya huo mrefu bila kuwapa shavu wasanii wa kike, Meneja wa Alikiba alikuwa  ni mwanamke, Seven Mosha ambaye licha ya juhudi binafsi za msanii mwanamama huyu alichangia kumpatia mafanikio makubwa kimuziki.  

Wimbo huu mpya 'Yalaiti' ni wa sita kwa Alikiba kuachia kwa mwaka huu baada ya kutoa 'Mahaba,' 'La La La' ft. Kings Music, 'On Fire', 'Sumu' x Marioo na 'Huku' ft. Tommy Flavour.

Hata hivyo, Alikiba yeye alikuwa akishirikishwa na wasanii wa kike, miongoni mwao ni Nandy (Nibakishie), Maua Sama (Niteke Remix), Maud Elka (Songi Songi Remix) n.k.

Rekodi lebo yake, Kings Music tangu imeanza kusajili wasanii hajawahi kumsainisha  msanii wa kike, hadi sasa wasanii ambao tayari wamesaini ni K2ga, Tommy Flavour, Abdukiba pamoja Cheed na Killy waliojitoa na kutimkia Konde Music Worldwide yake Harmonize.

Utakumbuka Alikiba alivuma baada ya kuachia albamu yake ya kwanza, Cinderella (2007) chini ya G Records, zilifuata albamu nyingi kama Ali K4Real (2009) na Only One King (2021) iliyoshinda tuzo za muziki Tanzania (TMA) 2021 kama Albamu Bora ya Mwaka.

Mwaka 2017 Alikiba aliandika rekodi kama msanii wa kwanza aliyesainiwa Sony Music Entertainment Africa kwa video ya wimbo wake (Aje) kufikisha 'views' zaidi ya milioni 5 katika mtandao wa YouTube kitu kilichoisukuma  lebo hiyo kumpatia tuzo (plaque).