Mlela: Ninapenda maisha ya kiki

Muktasari:

  • Mwigizaji wa filamu  nchini Tanzania, Yusuph Mlela amesema anapenda maisha ya kiki, kwamba kila analolifanya katika jamii ni kwa ajili ya kiki.

Dar es Salaam. Mwigizaji wa filamu  nchini Tanzania, Yusuph Mlela amesema anapenda maisha ya kiki, kwamba kila analolifanya katika jamii ni kwa ajili ya kiki.

Ametoa kauli hiyo leo Jumanne Agosti 27, 2019 baada ya kuulizwa na Mwananchi kama kabla ya kufanya jambo lolote hupenda kutanguliza kiki ili jambo husika liweze kuteka vichwa vya mashabiki wa filamu nchini.

“Niseme tu ukweli napenda kiki, watu wanaonizunguka waelewe kila kitu ninachofanya ambacho kinakuwa na gumzo wajue ni kiki, kwa sababu najua kiki ndio huwafanya watu wawe na umakini wa kukufuatilia kabla ya kutaka kufanya kitu,” amesema Mlela.

Kauli ya Mlela imekuja siku chache baada ya kuibuka mjadala mtandaoni kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na mwigizaji mwenzake, Anna Exavery maarufu Ebitoke.

"Suala la Ebitoke na mimi kama ni kiki au wapenzi nitakuja kulizungumzia, kwa sasa siwezi kusema ni kiki au sio kiki,” amesema Mlela.