Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mpango wa Nora Fatehi kwa Rayvanny ni upi?

JIACH 01

Muktasari:

  • Nora mwenye asili ya Morocco, pengine kwa sasa ndiye msanii wa kimataifa ambaye ana ukaribu mkubwa zaidi na Rayvanny lakini kuna jambo linaloacha maswali kuhusu ushirikiano wao.

Dar es Salaam. Miaka sita iliyopita ndipo ulisikika wimbo wa kwanza kati ya staa wa Bongo Fleva, Rayvanny na Nora Fatehi, mzaliwa wa Toronto, Canada ambaye amepata umaarufu kutokana na  soko la filamu India (Bollywood).

Nora mwenye asili ya Morocco, pengine kwa sasa ndiye msanii wa kimataifa ambaye ana ukaribu mkubwa zaidi na Rayvanny lakini kuna jambo linaloacha maswali kuhusu ushirikiano wao.

Swali hilo linakuja baada hivi karibuni Nora Fatehi kuachia wimbo wake mpya, Champions (2026) akiwa ameshirikiana na Sanjoy kutoka Bangladesh pamoja na Rayvanny, mshindi wa tuzo ya BET 2017.

Video ya wimbo huo unaohamasisha kupambania ndoto kubwa imeshutiwa visiwani Zanzibar chini ya Director Fole X, mshindi wa Tuzo za Muziki Tanzania (TMA) 2023.

JIACH 01

Ndani ya saa 22 pekee tangu kuachiwa video hiyo, iliifikia rekodi ya kutazamwa (views) mara milioni 10 katika mtandao wa YouTube, hatua inayoonyesha jinsi wasanii hao walivyo na nguvu ya ushawishi. 

Wimbo huu mpya umepata mapokezi makubwa kulilo ule uliotangulia, Oh Mama! Tetema (2025) ambao video yake ndani ya saa 24 ilitazamwa YouTube zaidi ya mara milioni 7.4, na ndani ya siku 3 ndipo ikafikia milioni 10.

Kwa jumla hadi sasa Rayvanny na Nora wameshirikiana katika nyimbo tatu, Pepeta (2019), Oh Mama! Tetema (2025) na Champions (2026). Pepeta ulikuwa wimbo wa kwanza wa kimataifa kwa Nora kuiimba kwa lugha ya Kiingereza.

JIACH 05

Baada ya Pepeta kufanya vizuri, Nora alichaguliwa kushiriki kwenye wimbo uitwao Light The Sky (2022) ambao ulikuwa maalum kwa ajili ya Kombe la Dunia la FIFA 2022 nchini Qatar.

Ikumbukwe katika mradi huo Nora alishirikiana na wasanii wengine kama RedOne, Manal, Balqees na Rahma Riad.

Hata hivyo, nyimbo zote tatu zipo katika majukwaa ya kidijitali (digital streaming) yake Nora na mara zote yeye ndiye amemshirikisha Rayvanny pamoja na wasanii wengine!

Hivyo licha ya ushirikiano wa wawili hao kuwavutia mashabiki wengi, hakuna kazi hata moja tunayoweza kusema ni yake Rayvanny amemshirikisha Nora, bali mara zote yeye ndio huwa anashirikishwa.

JIACH 04

Pengine hilo linafanyika kutokana na ushawishi mkubwa ambao tayari Nora yupo nao duniani, hivyo kazi yoyote inayowekwa katika jukwaa lake la kidijitali au la lebo anayofanya nayo kazi ya T-Series inakuwa inapata mapokezi mazuri.

Mathalani video ya wimbo wao, Oh Mama! Tetema (2025) imewekwa katika chaneli ya YouTube ya T-Series ambayo ina wafutiliaji (subscribers) zaidi ya milioni 313.

Hivyo huwezi kuzungumza mafanikio makubwa ya wimbo huu bila kuitaja lebo ya T-Series ambayo ndio imesimamia mradi wote huo.

JIACH 03

YouTube chaneli ya T-Series iliyofunguliwa Machi 13, 2006 ikijikita huko India, ni ya pili duniani kwa kuwa na wafutiliaji wengi wa maudhui yake, hivyo kazi nyingi za filamu na muziki zinazopandishwa hapo mara zote hupata mamilioni ya watazamaji.

Hiyo ni moja ya sababu kwa nini video ya wimbo huo ilifanya vizuri pindi tu ilipoachiwa, na hadi sasa ikiwa ni miezi 10 tangu imetoka imeshatazamwa mara milioni 110. Huu ni mradi wa kwanza wa Rayvanny na Bongofleva kwa ujumla kupiga namba hizo ndani ya muda huo.

JIACH 02

Ikumbukwe T-Series ni lebo ya muziki na kampuni ya utayarishaji wa filamu ya Kihindi iliyoanzishwa na Gulshan Kumar Julai 11, 1983.

Inajulikana zaidi kwa muziki wa filamu za Kihindi na muziki wa Indi-pop, huku maudhui yake YouTube yakiwa yameshatazamwa mara bilioni 346.7. Hii ndio lebo kubwa zaidi ya muziki nchini India, ikiwa imeshikilia hadi asilimia 35 ya soko la muziki wa India.

Ingawa inajulikana zaidi kama lebo ya muziki, T-Series pia imetayarisha filamu zaidi ya 100 na kwa miaka mingi imejipambanua kama kampuni inayoongoza katika utayarishaji wa filamu za Kihindi.

Katika mazingira kama hayo, huwenda Rayvanny ameona ni fursa nzuri zaidi kwa nyimbo hizo kuwekwa katika mitandao ya T-Series na Nora.

Wimbo wao kwanza, Pepeta (2019), katika chaneli ya Nora umeshatazamwa zaidi mara milioni 95, ikiwa ni ya pili kwa Nora kufanya vizuri zaidi YouTube baada ya kupitwa na ile aliyomshirikisha Jason Derulo wa Marekani, Snake (2025).

Umaarufu wa Nora kwenye muziki ulianza baada ya kuonekana kwenye wimbo, Dilbar (2018) uliotumika katika filamu ya Satyameva Jayate. Wimbo huo ukawa hit kubwa na kumfanya Nora kuwa mmoja wa mastaa wanaotamba kwa kudansi kwenye nyimbo za Bollywood.