Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwendelezo filamu ya Yesu kutoka 2027

Muktasari:

  • Tofauti na matarajio ya wengi, filamu hiyo haitakuwa marudio ya toleo la mwaka 2004, bali itaendelea pale simulizi la kwanza lilipoishia, ikiangazia matukio ya siku tatu kati ya kusulubiwa kwa Yesu Kristo na kufufuka kwake.

Marekani. Miaka 22 baada ya kuitikisa dunia na kuvuna zaidi ya dola za Marekani milioni 612. Filamu maarufu ya Kikristo, The Passion of the Christ, inarejea na mwendelezo mpya uitwao The Resurrection of the Christ. Huku muongozaji wake, Mel Gibson, akithibitisha kukamilika kwa utayarishaji wake.

Tofauti na matarajio ya wengi, filamu hiyo haitakuwa marudio ya toleo la mwaka 2004, bali itaendelea pale simulizi la kwanza lilipoishia, ikiangazia matukio ya siku tatu kati ya kusulubiwa kwa Yesu Kristo na kufufuka kwake.

Kutokana na ukubwa wa simulizi hilo, filamu imegawanywa katika sehemu mbili. Sehemu ya kwanza itaanza kuonyeshwa Mei 6, 2027. Huku ya pili ikitarajiwa kutoka Mei 25, 2028. Usambazaji wa filamu hiyo utafanywa na kampuni ya Lionsgate.

Ripoti zinaeleza kuwa filamu hiyo imetumia zaidi ya dola za Marekani milioni 100 kwa teknolojia ya kisasa ya uandaaji wa picha. Hatua iliyochangia kuongezeka kwa bajeti yake.

Katika mabadiliko makubwa, muigizaji Jim Caviezel, aliyemcheza Yesu Kristo katika filamu ya kwanza, hatarudi kwenye nafasi hiyo. Nafasi ya Yesu sasa itachezwa na muigizaji kutoka Finland, Jaakko Ohtonen. Huku Mariela Garriga akichukua nafasi ya Maria Magdalena iliyowahi kuchezwa na Monica Bellucci.

Kabla ya kutolewa kwa mwendelezo huo, Lionsgate kwa kushirikiana na Fathom Entertainment watarudisha filamu ya kwanza ya The Passion of the Christ kwenye kumbi za sinema kuanzia Septemba 10 hadi 17 mwaka huu.

Toleo hilo litakuwa limeboreshwa kwa ubora wa picha za 4K na sauti ya Dolby Atmos, huku watazamaji wakipata pia nafasi ya kutazama vipande maalumu vya nyuma ya pazia vya filamu mpya inayotarajiwa kutoka mwaka 2027.

Kwa mafanikio yake makubwa ya kibiashara na umaarufu duniani, wachambuzi wa tasnia ya filamu wanautaja mwendelezo huo kuwa miongoni mwa filamu za Kikristo zinazosubiriwa kwa hamu zaidi katika historia ya sinema.