Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ndani ya Boksi: Kuna mawinga wa uzinzi!!!

Muktasari:

  • Tulikuwa maeneo ya kujidai sana. Ambayo husahaulisha kifo, madeni na kujivisha imani kwa ujasiri wa kipumbavu kwamba utaishi milele amina. Yaani vile unajikuta Trump na Putin kwa wakati mmoja. Umevimbiana!

Dar es Salaam. Ndani ya Jiji la mawe Mwanza. Mandhari, hali ya hewa na lafudhi ya watu wake. Ilikuwa burudani na utalii tosha. Pombe zilishuka kooni kitakatifu na kutuama maungoni kiinjilisti. Kimsingi ni pepo ya dunia kwa ile Kanda ya Ziwa.

Tulikuwa maeneo ya kujidai sana. Ambayo husahaulisha kifo, madeni na kujivisha imani kwa ujasiri wa kipumbavu kwamba utaishi milele amina. Yaani vile unajikuta Trump na Putin kwa wakati mmoja. Umevimbiana!

Mie nilikuwa mpenzi mtazamaji, mshikaji wangu akiwa na Delila wake. Mrembo sana sana. Sura, rangi, sauti, umbile, macho hata ile ladha yake ya ulimi akiongea. Angeweza kukubariki vizuri bila kumtegemea Mwakasege. Huyu ni Magdalena wa kisasa.

Ningekuwa Rais wa nchi, noti zote ningeweka picha ya huyu mrembo. Ukiambiwa ni mke wa mtu hapo hapo ungejiombea ufariki. Alichokuwa anafanya na rafiki yangu pale tulipo ilikuwa ni aibu. Hawezi kufanya mke ama dem wa mtu.

Ukiambiwa ni mama wa watoto wawili ungezimia. Ungeoneshwa kitambulisho chake cha kazi. Ni wazi ungetamani uhame nchi. Na ungetajiwa na elimu yake, ni wazi ungezimia kwa mshtuko. Alikosa nini katika maisha yake? Hilo ndo swali la msingi. 

Fred alimpata Irene kupitia kwa rafiki wa Irene. Huyo rafiki wa Irene pia ni rafiki wa Fred. Kwa sababu alijua shida za Irene, na alijua tabia za Fred. Akaona bora awakutanishe. Fred ni mshikaji wangu ambaye anaishi kizinzi miaka yote.

Ndoa nyingi ni kaa la moto. 

Watu husherekea siku moja ya harusi tu. Hutaabika miaka mingi ndani ya ndoa. Usione wanandoa wako rodini wakicheka. Mioyo imeficha mengi sana. Na huyu alikuwa ni mmoja kati ya walio na ndoa zenye asili ya kuzimu.

Kama kuachana ingekuwa kitu cha sifa. Sherehe za kuachana zingekua nyingi kuliko sherehe za kuoana. Mwanamke hutazamwa kwa muonekano wa nje siku hizi. Siyo tabia. Umbo na sura basi, hata kama tabia imeoza haifai kabisa. Utajua mwenyewe mradi ama ngisi.

Ukiingia kiboya utalia na kusaga meno. Wanawake wazuri bado wapo, tatizo wanaharibiwa na mazingira yao. Wanawake pia husema wanaume ni matapeli. Sikatai, siku zote tapeli anamuona mwenzake ndiye tapeli. Hakuna namna tena.

Wanawake ni ‘matiriolistiki’. Ndio maana ndoa nyingi za kujionesha na hazidumu. Kwa mioyo ya leo wanawake ndoa kwao ni akaunti nene, ndinga kali, mjengo flan wa maana. Na hao ndo wengi zaidi dunia ya sasa. Una nini wewe kapuku? Chora usepeee.

Sura, umbo na mavazi ni hoja japo siyo sababu kuu. Hatufanani mitazamo ya vigezo vya kupata mwanamke. Kila mwanaume na vigezo vyake vidume huvutiwa na muonekano wa kike kwanza. Na baadaye ndo suala mtambuka la tabia linakuja. Tunapenda kwa kuona kwanza.

Na hapa ndipo wanadanganyika.
“Totozi’ nyingi hudhani shepu ni tiketi ya ndoa au kupata bwana mwenye pesa. Kuolewa hakuna kanuni ni bahati. Na mabadiliko ya mwanamke juu ya kuolewa ni sawa na mwanamume juu kuoa. Ni kesi moja hakimu tofauti. 

Jiheshimu, vaa vizuri sio kila mtu aone kiuno au kitovu. Kuwa na staha. Kwa sasa penzi na taasisi ya ndoa vimepoteza muelekeo.

Siyo wanaume siyo wanawake, wengi wao miaka ya hivi karibuni hawajui wanalolitaka. Wapo tu kama mvua za vuli. 

Na kuna mawinga wa ndoa hao. 
Hawa ndo nuksi kinoma mazee. Achana na mawinga wa Kariakoo kuna mawinga wa ndoa. Siyo poa jombaa, ‘waifu’ anapandiwa dau. Bebi wako anauzwa kama vijora na mabeseni ya Karikoo. Hawa hawafai.

Na nikuambie ukweli, mawinga ni madalali. Wanakula pesa za bosi na mpangaji. Yaani yule mwenye nyumba anamtumia dalali wake kutafuta wapangaji wa chumba chake. Chumba cha kuingia na kutoka tu. Yaani ukiliona danga huko niunganishe shosti.

Mke wa mtu anampanga winga, amtafutie mpangaji wa utupu wake. Siyo kwamba amekosa kitanda wala chakula anadanga ili akalipe vikoba. Kausha damu au kumtuza shost wake kwenye “kicheni pate’ uswazi huko. 

Hekeheka za kutaka kijora kipya, msuko mpya, mafuta ya Niffa na ‘smati fone’. Mke wa mtu anaona anachoachiwa na mume kidogo anaamua kudanga. Hawezi toka kwenda kujiuza, sasa wanatumia mawinga wa uzinzi kujiuza kwa mfumo mama. 

Winga ni dalali na kuwadi kwa wakati mmoja. Usikariri kwamba winga ni yule anayeleta bidhaa za viatu, mashati na matakataka ya Kariakoo tu. Kuna winga kibao kitaa zinauma wake za watu na waume za watu kuwadalalia kwa watu. ‘Veri badi’. 

Zamani ndoa zilidumu sana kwa sababu mambo hayakuwa mengi. Walio wengi kwa wakati ule, waliachana kwa uchawi, kutopika vizuri, kukosa adabu iwa wakwe na vitu dizaini hiyo. Lakini leo ndoa zilizo nyingi hufa kwa sababu moja tu. Uzinzi. Ni uzinzi tu. 

Unakuta mwanamke kutwa yupo kanisani. Kutwa kajitanda baibui na mitandio. Lakini kutwa kucha anachati uzinzi na kwenda kuzini uzinzini. Yaani kuzini kwa sasa ni kwenda saloni au bar na kurudi homu. Watu wanazini nyie.

Yaani katika dhambi ambayo yule bro shetani hata yeye anaikana. Kwa sababu inafanywa sana na wafuasi wake basi ni kuzini. Nyie watu waasherati mpaka uasherati wenyewe hautaki. ‘Jasti imejini’ hadi mawinga wa uzinzi wapo. Fred alimpata Irene kwa msaada wa winga. 

Mawinga mpo?