Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nyuma ya pazia Alikiba kuja na EP badala ya albamu

Muktasari:

  • Alikiba alivuma kimuziki baada ya kuachia albamu yake ya kwanza, Cinderella (2007) chini ya G Records, kisha zilifuata nyingine mbili, Ali K4Real (2009) na Only One King (2021) iliyotoka kwa ushirikiano wa Ziiki Media na Kings Music

Dar es Salaam, Staa wa Bongo Fleva, Alikiba, 37, anatarajia kuachia Extended Play (EP) yake ya kwanza, Starter (2024), tangu ameanza muziki lakini hatua hii tunaweza kusema ni kukwepa mtego wa kuhukumiwa na mafanikio ya albamu yake ya mwisho.

Alikiba alivuma kimuziki baada ya kuachia albamu yake ya kwanza, Cinderella (2007) chini ya G Records, kisha zilifuata nyingine mbili, Ali K4Real (2009) na Only One King (2021) iliyotoka kwa ushirikiano wa Ziiki Media na Kings Music.

EP hiyo mpya itatoka Septemba 14 ikiwa na nyimbo saba na kushirikisha wasanii watatu ambao ni Marioo, Nandy na Jay Melody ambaye naye mwaka huu ametoa albamu yake ya kwanza, Therapy (2024) yenye nyimbo 14.

Wasanii wengine Bongo waliotoa EP mwaka huu ni Anjella ‘The Black Queen’, Rayvanny ‘ZiiBeats Vol.2’, Bwana Misosi ‘Mbona Kimya’ n.k, huku albamu wakiwa ni Roma ‘Nipeni Maua Yangu’, Harmonize ‘Muziki wa Samia’, Young Lunya ‘Mbuzi’ n.k.

Ikiwa Alikiba, mwanzilishi wa Kings Music angekuja na albamu, ni wazi mashabiki wangeanza kuilinganisha na Only One King (2021) kutokana na sababu zifuatayo.

Mosi, albamu hiyo ilishinda tuzo za muziki Tanzania (TMA) 2021 kama Albamu Bora ya Mwaka, na kwa ujumla ilimuwezesha Alikiba kuondoka na tuzo tano na kuweka rekodi kama msanii aliyeshinda tuzo nyingi kwa msimu huo.

Katika kinyanganyiro hicho, Only One King ilizibwaga albamu kama ‘High School’ yake Harmonize, ‘Ona’ ya Marco Chali, ‘Live

At Sauti za Busara’ ya Wakazi na ‘Air Weusi’ ya kundi la Weusi.  
Utakumbuka Alikiba ndiye msanii pekee Bongo aliyeshinda tuzo zaidi ya tano na kuwa kinara katika misimu miwili tofauti ya tuzo za TMA zilizoanzishwa na Baraza la Sanaa Taifa (Basata) mwaka 1999, Kiba alifanya hivyo msimu wa 2015 na 2021.

Pili, ilitoa nyimbo kali kama ‘Jealous’ na ‘Utu’ ambao video yake ilikuwa ya kwanza kwa Alikiba kufikisha ‘views’ milioni 20 YouTube kwa mwaka mmoja, na sasa ikiwa na milioni 28 inashika nafasi ya tatu kama video yake iliyotazamwa zaidi katika mtandao huo.

Ni albamu iliyoshirikisha wasanii kama Abdukiba, K2ga na Tommy Flavour wote kutokea Kings Music, wengine ni Sarkodie (Ghana), Blaq Diamond (Afrika Kusini), Patoranking, Rudeboy na Mayorkun (Nigeria), Sauti Sol, Nyashinsksi na Khaligraph Jones (Kenya).

Tatu, Alikiba alitoa video za nyimbo nane za albamu hiyo ambazo ni Infidele, Ndombolo, Salute, Jealous, Oya Oya, Bwana Mdogo, Utu na Niteke, hivyo kuandika rekodi kama albamu iliyotoa video nyingi kwa mwaka huo.

Only One King ilizizidi albamu kama Sound From Africa (Rayvanny), Defination of Love (Mbosso), High School (Harmonize), Air Weusi (Weusi), 20 (Lady Jaydee), Asante Mama (Dogo Janja), Experience (Stereo), The Gift of Life (Best Naso) n.k.

Na ukiachana na hayo, pengine Alikiba ametoa EP ili kuweka mambo sawa na mshindani wake kimuziki, Diamond Platnumz ambaye tayari ametoa albamu tatu na EP moja.

Diamond, mwanzilishi wa WCB Wasafi tayari ametoa albamu kama Kamwambie (2010),  Lala Salama (2012) na A Boy From Tandale (2018), huku EP ikiwa ni First of All (2022) iliyotoka kwa ushirikiano wa Warner Music Group na WCB Wasafi.

Ikumbukwe msimu uliopita albamu ya Barnaba, Love Sounds Different (2022) ndiyo ilishinda tuzo ya TMA 2022 kama Albamu Bora ya Mwaka baada ya kuzibwaga, ‘The Kid You Know’ ya Marioo, ‘Made For Us’ ya Harmonize, ‘Street Ties’ ya Conboi na ‘Romantic’ ya Kusah.