Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Safari ya Maurice Sam anayetikisa kwenye filamu Nigeria

Muktasari:

  • Si kwa sababu ya uigizaji wake pekee, bali pia uwezo wake wa kutumia majukwaa ya kidijitali hususan YouTube kuwafikia mashabiki wake duniani. Jambo ambalo limekuwa likimtofautisha na waigizaji wengine

Nigeria. Katika kipindi ambacho tasnia ya Nollywood inaendelea kukua kwa kasi, huku ikivuka mipaka ya Afrika, Maurice Sam ni jina ambalo limekuwa likitajwa mara kwa mara kama miongoni mwa waigizaji wanaokuja kwa kasi katika tasnia ya uigizaji nchini Nigeria.

Si kwa sababu ya uigizaji wake pekee, bali pia uwezo wake wa kutumia majukwaa ya kidijitali hususan YouTube kuwafikia mashabiki wake duniani. Jambo ambalo limekuwa likimtofautisha na waigizaji wengine.

Maurice Sam, ambaye jina lake kamili ni Maurice Samuel Oluwaseun, alizaliwa Machi 12, 1990 jijini Lagos, Nigeria. Alihitimu Shahada ya Mass Communication katika Chuo Kikuu cha University of Lagos, ambapo akiwa chuoni alianza kujihusisha na utengenezaji wa maudhui ya kawaida kabla ya kujikita zaidi katika uigizaji.

Safari yake ya uigizaji ilianza rasmi baada ya kuhitimu masomo yake.Ambapo alianza kuonekana katika tamthilia ya televisheni ya Hustle, akicheza kama Acid nafasi iliyompa umaarufu mkubwa na kumtambulisha kwa mashabiki wengi.

Kupitia kazi hiyo, alifanikiwa kujijengea jina ndani ya Nollywood na kuanza kupokea fursa mbalimbali kutoka kwa watengenezaji filamu. Alipewa nafasi nyingi za kuigiza katika filamu za mapenzi na drama. 

Umaarufu wake uliendelea kuongezeka baada ya kuhamishia nguvu zake kwenye YouTube. Ambako alianzisha chaneli yake iliyomuwezesha kufikia mashabiki wengi zaidi.

Kupitia chaneli hiyo inayojulikana kama 'Maurice Sam TV', amefanikiwa kukusanya zaidi ya wafuatiliaji milioni 2.4. Huku baadhi ya filamu zake zikitazamwa zaidi ya mara milioni 10 ndani ya muda mfupi. 

Hatua hiyo imekuwa sehemu ya mabadiliko makubwa katika tasnia ya filamu Nigeria. Wasanii mbalimbali akiwemo Uche Montana wameanza kuzalisha na kusambaza kazi zao wenyewe kupitia majukwaa ya kidijitali bila kutegemea njia nyingine

Mbali na kuwa mwigizaji, pia Morice ni mtayarishaji wa filamu na mwandishi wa stori. Baadhi ya kazi zake amekuwa akiziongoza na kuziandika mwenyewe, lakini muda mwingine hufanya kazi na waandaji wengine ili kuandaa kitu kilichobora zaidi.


Tuzo alizofanikiwa kupata 

Kama waswahili wasemavyo mcheza kwao hutunzwa, kwa upande wa Maurice nguvu zake hazikwenda bure amewahi kutambulika na kunyakuwa tuzo mbalimbali ikiwemo Africa Magic Viewers’ Choice Awards. Akichukuwa mwigizaji bora katika tamthilia ya ‘Hustle’. Ushindi huo ulimuweka katika ramani ya wasanii wanaokuja kwa kasi katika tasnia hiyo. 

Hali ya mahusiano

Licha ya mafanikio hayo, maisha yake binafsi hasa ya kimapenzi yameendelea kuwa siri. Maurice ni miongoni mwa wasanii wanaopendelea kuweka faragha maisha yao nje ya kazi. 

Hali hiyo imepelekea kuhusishwa kutoka kimapenzi na mastaa mbalimbali akiwemo Sonia Uche, Mary Lazarus, Uju Okoli pamoja na Queen Nwokoye. Ingawa hakuna hata mmoja aliyewahi kuthibitishwa kuwa katika uhusiano naye. 

Mpaka kufikia sasa ameshaachia filamu mbalimbali katika chanel yake ikiwemo Mom First, The Love You Gave, Blood Sisters, Love and Crown, In His Arms, Accidental Bride, Half In Half, Thug Love 2, The Interview akiigiza na Uche Montana na nyinginezo.