Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sheik Walid aibua mapya ndoa ya Diamond, Zuchu

Muktasari:

  • Shekh Walid amekiri kuwafungisha ndoa Diamond na Zuchu huku Khadija Kopa akitoa sababu ya kutohudhuria.

Dar es Salaam. Licha ya kuwa jana Juni 2,2025 Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Walid Kawambwa wakati akizungumza na Mwananchi hakutaka kuongelea suala la ndoa ya mastaa wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul maarufu Diamond na Zuhura Othman marrufu Zuchu hatimaye kiongozi huyo wa dini amethibitisha kuwafungisha ndoa wawili hao.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumanne Juni 3, 2025 Walid amesema, amewafungisha ndoa miezi mitano iliyopita, ila habari za kuachana yeye hazifahamu.

"Kwanini watu wanapenda watu wengine wazini, Diamond na Zuchu ni kweli nimewafungisha ndoa mimi  toka miezi mitano iliyopita, ila hilo swali lako unaloniuliza kuhusu wameachana mimi silifahamu, sababu kama wangekuwa wameachana Diamondi angekuja kuniambia mimi.

"Vile mlivyoona kwenye mitandao ni kweli ndoa wala sio kiki, ila naona watu wengi wameshtushwa na hii habari, maana mmezoea kuwasema sema Diamond na Zuchu wazini kila kukicha sasa hili jambo la kheri lishangilieni na kuliombea kheri," amesema Walid

Aidha Walid hakutaka kuzungumzia hatua zilivyoanza hadi akatafutwa kuwafungisha ndoa Diamond na Zuchu na kwa nini ilikuwa siri.

"Mimi sitaki kuzungumzia chochote kile, swali lako nishakujibu kuwa kweli wamefunga ndoa, hayo mambo mengine ya kiundani zaidi sio jukumu langu kuwaelezea," amesema

Naye Khadija Kopa mama wa Zuchu ambaye naye awali alidai hata yeye ameona tukio hilo kwenye mitandao ya kijamii, leo ametoa sababu ya kutokuhudhuria ndoa hiyo.

“Zuhura ameolewa na Diamond japo walifanya siri lakini ni jambo la kheri, kuhusu kutohudhuria kwenye ndoa sisi kama wazazi, mimi na baba yake Zuhura tulishatoa  ruhusa  kama akitaka kufunga ndoa basi afunge tu hata kama sisi hatukuwepo kiufupi tulitoa baraka zote kwa mtu yeyote atakaye mpata, na vizuri kampata mtu wamefunga ndoa kisirisiri yote kheri,” amesema na kuongeza

"Nimeona kuna watu wanasema kwa nini Shekhe Walid amemshika mkono Diamond na sio Baba yake Zuhura, unajua sisi kama sisi waislamu wakati wowote Shekhe wetu anaweza kuwa Walii kwa upande wa mtoto.

“Na sisi tulishatoa ruhusa  kwa Sheikh Walid kuwa ndio baba yake wa hapa anayemsimamia , hivyo wakati wowote akiwa na jambo la ndoa  kwa mtu yeyote Zuhura  aende tu kwa Sheikh Walid, na kingine mimi Zuhura nilimzaa nikiwa siko kwenye ndoa, hivyo kama kuozeshwa angeozeshwa na kaka yake," amesema Khadija Kopa.