Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Swahili Fashion Week yazinduliwa, yagusa nishati safi ya kupikia

Muktasari:

Wiki ya maonyesho na Tuzo za Mitindo za Swahili kufanyika  Desemba 6 hadi 8, 2024. Ikijikita kwenye nishati safi ya kupikia

Dar es Salaa. Mwanzilishi wa Swahili Fashion Week Mustafa Hassanali amesema jukwaa hilo lililoanzishwa kwa lengo la kukuza wabunifu na wanamitindo linaungana na Rais Samia Suluhu Hassan katika kukuza uelewa juu ya matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Desemba 2,2024 wakati wa ufunguzi wa msimu wa 17 wa wiki ya maonyesho na Tuzo za Mitindo za swahili litalofanyika Desemba 6 hadi 8, 2024, amesema miaka 18 iliyopita Tanzania kulikuwa na wabunifu wachache ndiyo maana akapata wazo la kuanzisha jukwaa hilo.

"Wazo lilitokea kwamba tutengeneze jukwaa kwa ajili ya wabunifu wetu na hilo jukwaa lilitokea kwa sababu ya changamoto, mimi binafsi nilikuwa napata kwa ajili ya kuonesha nguo zangu. Vilevile jukwaa lilitengenezwa kwa ajili ya wabunifu waweze kupata fursa za kuonesha kazi zao.

Swahili Fashion Week jina lilitokea kwa sababu ya kuwapatia fursa wabunifu kutoka nchi ambazo zinazungumza kiswahili kuanzia Tanzania, nchi jirani na kuendelea duniani,"amesema Mustafa

Hata hivyo kwa mwaka huu 2024 wiki ya maonyesho na tuzo za Mitindo za swahili litafanyika Desemba 6 hadi 8 katika ukumbi wa Parthenon Hall/Greek Hellenic Club. Huku zaidi ya wabunifu wa mitindo 40 kutoka Tanzania na nje ya mipaka wakionyesha kazi zao.