Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tetema kwenye utatu wa nguvu

Muktasari:

  • Wimbo huo, ambao umetoka siku tisa zilizopita, hadi sasa YouTube umefikia jumla ya watazamaji milioni 16, ukiweka rekodi ya ngoma iliyofanya vizuri ndani ya saa 24 duniani.

Dar es Salaam. Wimbo  "Ooh Mama Tetema" ni kati ya kazi zilizowakutanisha wasanii watatu wa kimataifa: Rayvanny mwenye wimbo, Shreya Ghoshal kutoka India, na Nora Fatehi mwenye asili ya Morocco aliyekulia Canada. Na huo ndiyo utatu .

Wimbo huo, ambao umetoka siku tisa zilizopita, hadi sasa YouTube umefikia jumla ya watazamaji milioni 16, ukiweka rekodi ya ngoma iliyofanya vizuri ndani ya saa 24 duniani.

Hapa tunakuletea wasanii walioshiriki kwenye wimbo huo ambao uliachiwa kwa mara ya kwanza mwaka 2019 Vanny Boy akishirikiana na Diamond Platnumz.


Nora Fatehi

Mwanadada huyo kwenye ngoma ya 'Ooh Mama Tetema' alifanya kazi tatu  dansa ambaye alitunga stepu, mwimbaji aliyeimba mstari wa pili, na mrembo kwenye video hiyo. Asilimia kubwa ya kazi zake ni kucheza na kuigiza kwenye filamu mbalimbali, lakini mara chache amekuwa akiimba ingawa si mzuri kwenye hilo.

Ukiachana na Ooh Mama Tetema na Pepeta ambazo zote aliimba na Rayvanny, Nora pia alifanya kolabo na Jason Derulo mwaka huu kwenye ngoma ya Snake iliyofanya vizuri YouTube.

Asilimia kubwa ya mashabiki wanafahamu msanii huyo anatokea India kutokana na kuigiza kwenye filamu nyingi za Bollywood, ikiwemo Tigers of the Sundarbans ya mwaka 2014.

Lakini ukweli ni kwamba Fatehi alizaliwa na kukulia Toronto, Canada mwaka 1992, na ana asili ya Morocco. Alihitimu Shule ya Msingi ya Westview Centennial huko Toronto. Alisoma Sayansi ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa katika Chuo Kikuu cha York, Marekani.

India ni sehemu yake ya makazi na amekuwa akiipenda nchi hiyo tangu akiwa mtoto. Kwenye moja ya mahojiano yake aliwahi kusema anajiona kuwa ni Mhindi wa moyo akimaanisha nchi hiyo iko moyoni mwake, na hiyo ndiyo sababu wengi hudhani anatokea huko. Kati ya kazi zake maarufu aliigiza kwenye filamu ya Dilbar (2018), Saki Saki's True (2024), Nora (2024), Body On Me (2024), Who's Your Mommy (2024) na Light the Sky (2022).


Shreya Ghoshal

Huyu ni msanii mwingine aliyeshirikiana na Rayvanny, na ameimba wimbo huo kwa ukubwa kuanzia mstari wa mwanzo hadi mwisho kwenye kimalizio.

Hii inakuwa mara ya kwanza kwa Rayvanny kuimba na mwanamama huyo kwenye kolabo zake za kimataifa, lakini inakuwa ya pili kutoka India baada ya Pepeta.

Ni mwimbaji kutoka India akiwa miongoni mwa waimbaji wenye ushawishi mkubwa na waliobobea zaidi katika Bara la Hindi. Anajulikana zaidi kwa sauti yenye upana na uwezo wa kuimba katika mitindo mbalimbali. Nchini India wanamuita "Malkia wa Mabadiliko ya Sauti" kutokana na uwezo wa kipekee wa kuimba kwa hisia.

Ghoshal amerekodi nyimbo kwenye filamu katika lugha mbalimbali za India na za kigeni, na ameshinda tuzo nyingi zikiwemo Filmfare Award for Best Female Playback Singer kupitia filamu ya Deewani Mastani. Alianza kurekodi wimbo kupitia wimbo Ganraj Rangi Nachto ambao ni toleo la wimbo maarufu uliowahi kuimbwa na Lata Mangeshkar.

Albamu yake ya kwanza ilikuwa Bendhechhi Beena, iliyotoka Januari 1998 ikiwa na nyimbo 14. Albamu nyingine ni O Tota Pakhi Re, Ekti Katha (1999), Mukhor Porag (2000), Rupasi Raate (2002), Krishna Bina Ache Ke (2007).

Baadhi ya kolabo za kimataifa alizowahi kufanya mkali huyo wa sauti ni pamoja na Yimmy Yimmy aliyoshirikishwa na Tayc kutoka Ufaransa, Zaalima alioshirikishwa na Dystinct wa Morocco, na Guli Mata aliyoimba na Saad Lamjarred, Jennifer Winget na Anshul Garg.