Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ukaribu wa Kim Kardashian na Hamilton washtua mashabiki

Muktasari:

  • Kuonekana kwa wawili hao kumezidi kuchoche tetesi zinazodai kuwa wapo kwenye uhusiano wa kimapenzi.

Marekani. Staa wa Marekani Kim Kardashian na bingwa wa mashindano ya magari ya Formula One Lewis Hamilton wameendelea kuzua gumzo mitandaoni baada ya kuonekana pamoja jijini Tokyo, Japan.

Kuonekana kwa wawili hao kumezidi kuchoche tetesi zinazodai kuwa wapo kwenye uhusiano wa kimapenzi.

Kwa mujibu wa picha na video zilizosambaa mitandaoni, wawili hao walionekana wakifurahia matembezi mitaani huku wakitabasamu na kuwasalimia mashabiki waliokuwa wakiwashangaa.

Hiyo siyo mara ya kwanza kwa wawili hao kuonekana pamoja wamewahi kuonekana katika matukio mbalimbali, ikiwemo mchezo wa Super Bowl pamoja na katika hoteli ya kifahari nchini Uingereza, jambo lililozidi kukuza madai hayo.

Hata hivyo, Hamilton aliwahi kuulizwa ukaribu wake na Kardashian, lakini alisema suala hilo ni la maisha yake binafsi na hataki kulizungumzia hadharani.

Hamilton ni nani?

Lewis Hamilton ni bingwa wa mbio za magari duniani anayeshiriki mashindano ya Formula One. Raia huyo wa Uingereza anatajwa kuwa miongoni mwa madereva bora kuwahi kutokea, akiwa ameshinda ubingwa wa dunia mara saba rekodi inayomuweka sambamba na vinara wengine wa mchezo huo.