Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Usiyoyajua kuhusu Munishi, angulo lake

Muktasari:

  • Licha ya wimbo wake huo kumtambulisha kwenye jamii, nyimbo zake nyingi zilikuwa zikipendwa sana hasa hapa nchini na nchi ya Kenya ambako ndipo aliporekodia nyimbo zake hizo

Moshi. "Nahuzuni moyoni, mimi siimbi nalia, namlilia Malebo, amekataa kuokoka, nilizoimba ni nyingi, nikimuonya Malebo, bado hajabadilika, sasa siimbi nalia"

Haya ni baadhi ya mashairi ya wimbo wa "Namlilia Malebo" ulioanza kutamba na kusikika kwenye vyombo mbalimbali vya habari vya ndani na nje ya Tanzania miaka ya 1980 ukiimbwa na msaani maarufu wa nyimbo za injili, Faustine Munishi (Malebo).

Munishi ambaye ni mkazi wa Wilaya ya Moshi, Mkoani Kilimanjaro na mwenye makazi yake nchini Kenya, alianza kutamba na nyimbo zake za injili ambazo zilimtambulisha ndani na nje ya Afrika Mashariki kutokana na namna yake ya uimbaji.

Licha ya wimbo wake huo kumtambulisha kwenye jamii, nyimbo zake nyingi zilikuwa zikipendwa sana hasa hapa nchini na nchi ya Kenya ambako ndipo aliporekodia nyimbo zake hizo.

Katika pitapita za Mwandishi wa Mwananchi, jicho  lilimnasa mwimbaji huyo akiingia kwenye moja ya mgahawa uliopo katikati ya mji wa Moshi na waliweza kupiga naye stori mbili tatu kuhusu maisha yake kwa sasa hasa katika soko la muziki wa injili.

Munishi alisema kipaji chake cha muziki kilianza kuonekana haswaa miaka ya 1980 baada ya kupata mwaliko kwenda nchini Kenya na kuanzia hapo ndipo nyimbo zake zilianza kuchezwa kwenye vyombo vya habari vya Kenya ikiwemo redio ya Voice of Kenya ambayo ndiyo iliyomuibua.

"Nilizunguka Tanzania kuimba nyimbo za injili, ilipofika mwaka 1982 ndipo nikapata mwaliko wa kwenda Kenya, kule Kenya wimbo wangu huu uliweza kuingia kwenye vyombo vya habari baada ya hapo Mtayarishaji mmoja wa muziki wa VOK (Voice of Kenya), aliomba nisiondoke kabla sijarekodi nyimbo zangu katika televisioni ya Taifa ya Kenya. 

"Miaka hiyo waimbaji wote wa Tanzania, akiwemo Baraka Mwishehe walikuwa wanasafiri mpaka Kenya kwa ajili ya kurekodi nyimbo zao kama mimi,"alisema mwimbaji huyo.

Safari yake ya muziki 

Alisema pamoja na kuwa na jina kubwa na kujijengea umaarufu mkubwa ndani na nje ya nchi za Afrika Mashariki anguko lake  la muziki linatajwa kutokea pale alipobadilisha vionjo katika nyimbo zake na kuzihusisha na masuala ya kisiasa kwenye mauaji ya halaiki ya Kimbari Rwanda mwaka 1994, akiimba wimbo wa

 "Mwokozi amenituma Rwanda niwaambie wawakaribishe wageni, niwaambie wapendane ndugu kwa ndugu, wasiuane."
Alisema baada ya kuimba wimbo huo, ulifungiwa kuchezwa kwenye chombo chochote cha habari.

"Changamoto kubwa niliyoipata ni ile ya kukosoa serikali ya Tanzania pia, nakumbuka wakati huo nyimbo zangu zilifungiwa na serikali. Kuna wimbo mmoja niliimba kwamba "

"Wakati huo ni kipindi ambacho kilikuwa na 'mauaji ya Kimbari ya Rwanda' na niliimba ule wimbo baada ya kuongozwa na roho mtakatifu kwamba yale yaliyotokea Rwanda yanaweza kutokea katika nchi yoyote ya Afrika kama siasa za nchi hazitaenda vizuri." 

“Nikatoa angalizo kwamba hata Tanzania tusipofanya siasa za haki na kuwatendea watu haki mlipuko uliotokea Rwanda unaweza kutokea Tanzania, wimbo ukafungiwa," Munishi..
"Na baada ya changamoto hiyo kutokea, vyombo vya habari na makanisa vikanichunia nikawa sisikiki tena Tanzania,” alisema.