Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wasanii Bongo Movie kujipima uwezo Rwanda

Muktasari:

  • Akizungumza na waandishi wa habari Baraka Chigele ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya A2V Television Studio, leo Agosti 6, 2024 jijini Dar es Salaam alisema tamasha hilo litafanyika nchini Rwanda huku likihusisha nchi zote za Afrika.

Dar es Salaam, Katika kukuza lugha ya Kiswahili kupitia vipindi vya runinga na filamu katika nchi za ukanda wa Afrika Mashariki hasa zile zisizozungumza lugha hiyo Kampuni ya A2V Television Studio, imeandaa tuzo za filamu za Kiswahili.

Akizungumza na waandishi wa habari Baraka Chigele ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya A2V Television Studio, leo Agosti 6, 2024 jijini Dar es Salaam alisema tamasha hilo litafanyika nchini Rwanda huku likihusisha nchi zote za Afrika.

"Tamasha litafanyika nchini Rwanda huku likihusisha nchi zote za Afrika ambazo zipo tayari kuleta filamu zao za kiswahili kuingia kwenye mashindano, lakini pia hata zile zilizopo nje ya Afrika zinaruhusiwa ziwe zimetumia lugha ya Kiswahili hata kwa udogo,"amesema Chigele. 

Imeelezwa kuwa mpaka sasa nchi 16 kutoka Afrika zimekubali kushiriki mashindano hayo na nchi mbili kutoka nje ya Afrika ambazo ni Canada na Ujerumani.

Kwa upande wake Jamal Mbaga, ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa mashindano hayo, amesema sababu ya kuanzishwa mashindano hayo ni kiswahili kwa sasa kuwa lugha ya kimataifa hivyo kuna haja ya kukitanua zaidi. 

"Katika lugha 10 zinazokua kwa kasi hapa Afrika lugha ya Kiswahili inaongoza hivyo kuna kila haja ya kukieneza zaidi na sisi tunataka kukieneza kupitia filamu za kiswahili kutoka Tanzania", amesema Jamal

Ameongezea kwa kusema ni muda wa wasanii wa filamu kutoka Tanzania kutengeneza kazi nzuri na zenye ubora ili kushindanishwa na wasanii wengine wa filamu duniani kote.

Hivyo basi wasanii wa filamu wa Tanzania wanaombwa kupelekea kazi zao kwenye mashindano bila ya kuogopa kwani ni mara ya kwanza kuanzishwa mashindano hayo, huku ikielezwa kwamba majaji watakaotoa maamuzi hawatakua na upendeleo wowote. 

Naye Hidaya Njaidi ambaye ni balozi wa mashindano hayo  amesisitiza wasanii wa kuigiza waende shule wasome juu ya kile wanachokifanya.

"Vyuo mbalimbali vipo tayari kupokea wasanii wa maigizo ili iwasaidie kuandaa kazi zenu kwa mashindano ya kimataifa," amesema Hidaya 

Wasanii wa maigizo wanaombwa kutumia vizuri nafasi hiyo kwani ni miongoni mwa sababu itakayosaidia kupelekea kazi zao kimataifa.

Mchakato mzima wa ukuzaji kiswahili, filamu na utoaji wa tuzo utasimamiwa na Wizara ya Sanaa Utamaduni na Michezo kupitia Baraza la Kiswahili la taifa na bodi ya filamu Tanzania.