Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yaliyojiri kumbukumbu mwaka mmoja kifo cha Kanumba

Muktasari:

Kanumba na filamu nchini

Kwa namna inavyoonekana ni kama hakuna mcheza filamu ambaye anaelekea kumrithi Steven Kanumba kwa umahiri au hata uwezo wa kutoa filamu kwa wingi. Hadi kifo kinampata Kanumba alikuwa akitoa filamu mpya kila baada ya muda mfupi, kuna wakati alikuwa akitoa hadi filamu kila baada ya miezi mitatu au hata chini ya hapo.Filamu zake nyingi bado zinaendelea kupendwa japo kwa baadhi ya watu wanaona zimeanza kupoa umaarufu wake, huku kukiwa hakuna mcheza filamu wa kumrithi.

Waigizaji wa filamu nchini nyuso zao bado zinaonyesha huzuni na woga wa kujaribu aliyofanya Steven Kanumba, licha ya mwaka mmoja kupita tangu kifo cha muigizaji huyo nyota kilichoadhimishwa Jumapili Aprili 7, 2013.

Kanumba aliyekuwa ameanza kufanya kazi na wasanii kutoka nchini Nigeria, Ghana, Hollywood ndoto zake zilikatishwa baada ya kifo cha ghafla kilichotokea Aprili 7 mwaka 2012, usiku wa saa sita nyumbani kwake Sinza Vatican jijini Dar es Salaam.

Siku ya maadhimisho ya kifo chake, waigizaji wengi na wasanii wengine walikusanyika Viwanja vya Leaders Club alfajiri wakitafakari namna siku hiyo iliyokuwa na majukumu mengi itakavyomalizika.

Saa tatu kamili msafara ulianza kuelekea Usharika wa KKKT Kimara temboni ambapo ilifanyika misa ya kumuombea marehemu pamoja na sadaka ya pekee iliyotolewa na familia pamoja na waigizaji wenzake.

Misa hiyo iliyofanyika kanisani hapo kwa saa tatu ilihudhuriwa na watu wengi akiwemo Elizabeth Michael maarufu kama Lulu anayetuhumiwa kumuua Kanumba, aliyeambatana na mama yake mzazi pamoja na waigizaji wapatao 100 hali iliyopelekea kanisa hilo kujaa kupita kiasi.

Waigizaji kutoka Ghana na Nigeria waliohudhuria ni pamoja na Ama na Nana walioambatana na aliyekuwa Meneja wa Kanumba, Prince Richard anayeishi nchini Marekani aliyefika nchini kwa ajili ya kuadhimsha siku hiyo pamoja na wasanii wengine.

Vicent Kigosi ‘Ray’, Irene Uwoya, Shamsa Ford, Johari, Jacob Steven ‘BJ’, Tino, Steve Nyerere, Rado, Mzee Chilo, Witness Lunyungu, Yusuph Mlela, Simon Mwakifamba ni baadhi ya waigizaji maarufu walisali katika kanisa hilo

Baada ya misa kulikuwa na chakula cha mchana kilichoandaliwa na mama wa Kanumba Frola Mtegoa kilicholiwa kanisani hapo. Msafara ulianza kuelekea makaburini Kinondoni ambapo aliyekuwa mpenzi wake Lulu aliweka shada la maua kwa mara ya kwanza pamoja na meneja wake Prince Richard.

Kwa  mara ya kwanza Lulu alibusu msalaba wa Kanumba na baada ya hapo alisema “Nina uchungu wa kufiwa na niliyempenda, sina jinsi imeshatokea siwezi kuzungumza lolote” alisema Lulu na baadaye alishikwa na mama wa Kanumba na kwenda kukaa mbali kidogo na kaburi hilo.

Majira ya saa mbili usiku shughuli ilihamia pale Leaders Club ambapo filamu yake ya mwisho Love & Power aliyoigiza na marehemu Sharomilionea ilizinduliwa rasmi.
Filamu nyingine iliyoandaliwa na Jackline Wolper pamoja na kampuni ya Steps Entertainment iliyoitwa After Death pia ilizinduliwa siku hiyo.

“Sisi kama familia kwa kushirikiana na wenzetu pamoja na kampuni ambayo marehemu alikuwa akifanya nayo kazi ya Steps tulipanga kumuenzi kwa kuzindua filamu yake ya mwisho kuigiza ya Love & Power lakini pia Jack Wolper alikuwa na tukio kama hilo ambapo amezindua filamu yake ya After Death kama ishara ya kumuenzi Kanumba,” anasema Seth Bosco mdogo wa Kanumba.

Itaendelea kesho