Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Zuchu, Diamond wameridhika au wamesusa?

Muktasari:

  • Waimbaji hao kutokea WCB Wasafi, wanaonekana kupunguza kasi upande wa kutengeneza na kutoa video za nyimbo zao ambazo zimekuwa zikipata mapokezi mazuri kutoka mashabiki wao.

Dar es Salaam. Ndivyo tunavyoweza kusema kwa namna mastaa wa Bongofleva, Zuchu na Diamond Platnumz wanavyosimamia muziki wao kwa wakati huu ikiwa ni takribani miaka sita tangu waanze kufanya pamoja.

Waimbaji hao kutokea WCB Wasafi, wanaonekana kupunguza kasi upande wa kutengeneza na kutoa video za nyimbo zao ambazo zimekuwa zikipata mapokezi mazuri kutoka mashabiki wao.

Ni zaidi ya miezi miwili tangu walipoachia wimbo wao, Inama (2025) uliotayarishwa na Laizer kutokea Wasafi Records lakini hadi sasa hawajatoa video yake, kitu kinachoibua swali iwapo wameridhika na mafanikio.

Inama (2025) ni wimbo wa mapenzi ambao wawili hao wanaimba kuhusu uhusiano wao uliosimama imara licha ya watu kutamani waachane kwa sababu zao binafsi.

Kwa ucheshi na maneno ya kujiamini, Zuchu anakiri kuwa hata yeye hawezi kumuacha mwenzake, hivyo kwa pamoja anachagua kucheza kwa kuinama na kuinuka ili kuonyesha furaha yao ilivyo kwa sasa.  

Licha ya wimbo huo kuufanyia challenge nyingi kupitia mitandao ya kijamii na kupokelewa vizuri, Zuchu na Diamond ni kama wameshindwa au hawana mpango wa kuachia video yake.

Huu unakuwa mwendelezo wa wao kutoa nyimbo nzuri bila video zake, kitu ambacho awali wakati wanaanza kushirikiana hakikuwepo ila baada ya Zuchu kupata umaarufu mkubwa kimuziki ndipo hayo yameanza.

Kabla ya Inama (2025), walishatoa nyimbo nyingine mbili, Raha (2024), na Wale Wale (2024) kutoka katika albamu ya kwanza ya Zuchu (2024), hizi nazo hadi leo video zake hazijaonekana machoni kwa mashabiki.

Hivyo nyimbo tatu za mwisho ambazo Diamond na Zuchu wameshirikiana hazijatolewa video zake!. Pengine tayari wameridhika na kazi ambayo walishaifanya hapo awali, kazi iliyokuwa na matokeo mazuri.

Ikumbukwe nyimbo zao tatu za mwanzo, Litawachoma (2020), Cheche (2020) na Mtasubiri (2022), zote video zake ziliachiwa na zimepata mamilioni ya watazamaji katika mtandao wa YouTube.

Mathalani video ya wimbo 'Mtasubiri' kutokea katika Extended Playlist (EP) yake Diamond, First of All (2022), imetazamwa YouTube zaidi ya mara milioni 44 ikiwa ni miaka mitatu tangu itoke.

Hata hivyo, video hiyo ilikuja kufungiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuchezwa katika vituo vya televisheni kutokana na kipande chake cha mwanzo kukiuka maadili, hivyo walitakiwa kukirekebisha.  

Kufuatia hilo, tangu wakati huo Diamond na Zuchu hawajatoa video yoyote ya wimbo walioshirikiana, hili nalo linaacha maswali ikiwa wameamua kususia upande huo!.

Wanarekodi pamoja na wimbo unatoka mzuri tu, kisha wanafanya challenge za kutosha lakini video rasmi ya wimbo husika ndio hawatoi. Je, wameridhika au wamesusa?.

Katika video ya wimbo wa Zuchu, Utaniua (2022), Diamond ametokea na kucheza uhusika kama mpenzi wake na ni kazi nzuri iliyovutia ila huo hakuwa wimbo walioshirikiana kama hizo nyingine.

Video hiyo hadi sasa imetazamwa zaidi ya mara milioni 35, na hakuna video ambayo wametoa pamoja ambayo haijafanikiwa kutazamwa zaidi ya mara milioni 30. Hii inaonyesha kazi zao zinavutia wengi lakini wamechagua kusimama kutoa video. 

Tangu wametangaza kufunga ndoa, hawajatoa video yoyote ya muziki. Ilitegemewa wimbo, Inama (2025) ndio itakuwa ya kwanza kufanya hivyo ila hadi wakati huu bado hilo halijatokea. 

Ikumbukawe Diamond ndiye alimtoa Zuchu kimuziki kupitia lebo yake, WCB Wasafi ambayo mwaka 2015 ndipo ilianza kutambulisha vipaji vipya katika muziki.

Zuchu, mziwanda wa Malkia wa Taarab, Khadija Kopa, alitambulishwa kupitia EP yake, I Am Zuchu (2020) yenye nyimbo saba, huku akiwashirikisha wasanii wawili, Mbosso na Kopa.

Tangu kuchomoza kwa jina lake katika Bongofleva, ndiye mwanamuziki wa kike aliyeshirikiana zaidi na Diamond wakitoa nyimbo sita pamoja!.

Kwa sasa Zuchu anasimama kama chapa yenye ushawishi katika muziki akiweka rekodi mbalimbali, mathalani ndiye mwanamuziki wa kwanza wa kike Afrika Mashariki aliyetazamwa YouTube zaidi ya mara bilioni 1.

Na kwa ujumla, Zuchu amekuwa mwimbaji wa nne kutokea kwenye Bongofleva kufikisha 'views' bilioni YouTube akiwa ametanguliwa na Diamond, Rayvanny na Harmonize, mwanzilishi wa Konde Music Worldwide.