Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bei ya nyama yazidi kupaa

Muktasari:

Baadhi ya wafanyabiashara wa nyama walisema jana kuwa hivi sasa ng’ombe mmoja anauzwa kwa Sh400,000 badala ya Sh300,000.

Shinyanga. Bei ya nyama ya ng’ombe mkoani hapa imepanda kutoka Sh5,000 hadi 6,000, kutokana na mifugo kuadimika kwenye minada.

Baadhi ya wafanyabiashara wa nyama walisema jana kuwa hivi sasa ng’ombe mmoja anauzwa kwa Sh400,000 badala ya Sh300,000.

Wauzaji nyama, Hussein Shija na Onesmo Kwako, walisema ng’ombe wengi ni ndama ambao hawajafikia kiwango cha kuchinjwa.

Shija alisema licha ya kupanda bei ya ng’ombe, kwa sasa gharama za usafirishaji ni Sh10,000, ushuru 8,000 na kilo moja ya nyama 6,000 na kwamba faida inayosalia ni 15,000 kwa ng’ombe mwenye uzito wa kilo 70.

“Katika minada ya Mhunze Kishapu, Old Shinyanga na Tinde, ng’ombe wamekuwa adimu, hivi sasa tunanunua katika Mnada wa Iborogero wilayani Igunga, Mkoa wa Tabora lakini faida ni kidogo,” alisema Kwako.

Wakazi wa Shinyanga, walisema awali kilo moja ya nyama ilikuwa ikiuzwa Sh4,000 kwa kilo na kupanda hadi 5,000 na sasa imeongezeka tena hadi Sh 6,000.