BENKI ya Access yawashukuru wateja ikisherehekea miaka tisa
Muktasari:
Benki hiyo inayosherehekea miaka tisa ya huduma nchini tangu kuanzishwa kwake mwaka 2007 imefanikiwa kutanua huduma zake mikoa kadhaa nchini hivyo kuongeza idadi ya wateja inaowahudumia.
Dar es Salaam. Benki ya Access Tanzania imewashukuru wateja wake na wadau wengine kwa uaminifu tangu ianze kutoa huduma zake nchini.
Benki hiyo inayosherehekea miaka tisa ya huduma nchini tangu kuanzishwa kwake mwaka 2007 imefanikiwa kutanua huduma zake mikoa kadhaa nchini hivyo kuongeza idadi ya wateja inaowahudumia.
Mpaka sasa, ikiwa na zaidi ya wateja 270,000 tayari imetoa mikopo ya biashara yenye thamani ya Sh800 bilioni kwa zaidi ya wajasiriamali 84,000 wadogo na wa kati na kukuza amana zake ambazo thamani yake ni zaidi ya Sh144.7 bilioni.
Mkuu wa Idara ya Fedha wa benki hiyo, Julius Ruwaichi alisema: “Tunatoa shukrani za dhati kwa wateja wetu walioonyesha imani kwetu na wadau wote walituwezesha kufika tulipo leo. Tutaendelea kutoa huduma bora.”