Halimashauri Kusini zatakiwa kutenga bajeti za mbegu

Mtafiti wa mazao jamii ya mizizi ya viazi na mihogo kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (Tari) kituo cha Naliendele, Festo Masisila ameziomba Halmashauri kutenga bajeti za mbegu bora za mazao mbalimbali.

Muktasari:

  • Ili kuondokana na uhaba wa chakula katika mikoa ya Lindi na Mtwara Halmashauri zimeombwa kupanga bajeti ya mbegu bora za zao la muhogo ili kuongeza uzalishaji wa zao hilo.

Mtwara. Mtafiti wa mazao jamii ya mizizi ya viazi na mihogo kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (Tari) kituo cha Naliendele Festo Masisila, ameziomba Halmashauri kutenga bajeti za mbegu bora za mazao mbalimbali.

 Alisema kuwa muhogo umekuwa na msaada mkubwa hasa nyakati za njaa ambapo umekuwa ukiwasaidia wakulima kupata chakula, hivyo kuwa na mbegu za kutosha kunaweza kusaidia wakulima.

“Halmashauri tunaziomba ziendelee kupanga bajeti za kununua mbegu bora za mazao mbalimbali ikiwemo muhogo ambapo unaweza kutengeneza zaidi ya bidhaa 70 unaweza kutengnenza kwakutumia zao la muhogo,” amesema.

Aidha mtafiti huyo ameongeza kusema: “Muhogo unathamani kubwa unatumiwa kwa kiasi kiubwa ili tuzalishe kwa tija lazima tupate mbegu bora kwa kuzalisha eneo dogo lakini uzlaishaji mkubwa ambapo kwa hekali mbili na nusu unaweza kupata tani zaidi ya 22.”

Kwa mujibu wa Masisila, mbegu bora za muhogo huzaa mara tatu ya zile za asili na kwamba kutumia mbegu bora kunaweza kusaidia kuondokana na uzalishaji duni.

“Ili kupanda na kuzalisha kwa wingi angalau 20/30 tufikie asilimia 10 kwenye zao la muhogo, kwasasa mfano mbegu aina ya mkumba inazaa tani 50 kwa hekali mbili na nusu,” alisema Masisila 

Joseph Tesha Mkuu wa Divisheni ya Kilimo Mifugo na Uvuvi amesema kuwa haya majaribio wananchi yanawapa fursa kubwa zaidi ya kujifunza kwa kitendo ili waweze kujua ubora wa mbegu.

“Tunaambiwa kupata mashina 4000 kwa kilo moja hii inatupa picha kuwa pamoja na kufaa kwa chakula ni zao la bishara tija ni muhimu ili kile unachozalisha unazalisha kwa eneo dogo mavuno mengi yaani unapata kilo toshelevu kwa mbegu bora ambayo inaweza kutosha” alisema Tesha 

Naye Bakari Said mkulima wa zao la Muhogo kata ya Mkunwa alisema kuwa mbegu bora ni nzuri zinatofautiana hasa kwenye kuzaa na ujazo.

“Hizi mbegu bora na za asili zinatofautiana kwa kiwango kikubwa zipo ambazo ni bora zaidi ambazo tumezikubali na zingine nzuri kiasi. Mbegu aina ya kiroba inazaa kwa wingi zaidi inakomaa haraka na haishambuliwi na magonjwa”