Mkutano kujadili kuongeza watumiaji wa bima nchini waja

Mkutano kujadili kuongeza watumiaji wa bima nchini waja

Muktasari:

  • Chuo cha Bima ya Jamii Afrika na wadau wengine wameandaa mkutano utakaojadili mikakati ya kuongeza huduma za bima, ili kuisaidia Serikali kufikia lengo la asilimia 50 ifikapo mwaka 2030.

Dar es Salaam. Chuo cha Bima na Hifadhi ya Jamii Africa cha Dar es Salaam kimeandaa mkutano wa kwanza utakaowatanisha wadau ili kujadili mkakati wa kusaidia Serikali kuongeza huduma za bima nchini.

Lengo la Serikali ni kuhakikisha huduma za bima zinawafikia wananchi kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2030.

Mbali na mkakati wa kuongeza huduma ya bima, mkutano huo utaofanyika Aprili 16 jijini Dar es Salaam, utajadili jinsi sekta ndogo ya bima inavyoweza kuongeza mchango katika Pato la Taifa (GDP) na changamoto na fursa za bima za benki.

Akizungumza jana, mwenyekiti mtendaji wa chuo hicho Dk Baghayo Saqware mkutano huo unafanyika kwa mara jijini Dar es Salaam, ambapo pia watu zaidi ya 100 watashiriki kupitia teknolojia ya Zoom.

"Kama chuo kikuu tuna jukumu la kuunga mkono lengo la serikali la kufikia lengo kwa hivyo tumekuwa na majukwaa tofauti ambayo yanalenga kuwakutanisha wadau wote wa bima pamoja na kampuni na taasisi zinazofanya kazi na bima ili watu waweze kubadilishana mawazo na

uzoefu, " alisema

Alisema lengo la mkutano huo niĀ  kuhakikisa chaneli za bima zinafika nane na kuboresha zilizopo.

Hata hivyo alisema ili huduma za bima zinawafikia wananchi wengi, lazima kampuni za bima ziendeshwe kwa kutumia mawakala.