Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Shayiri yachochea uzalishaji vileo ‘bia’, Konyagi yaongoza mauzo TBL

Muktasari:

  • Uzalishaji wa shayiri nchini umechangia ukuaji wa sekta ya bia, huku Konyagi ikiongoza mauzo ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) mwaka 2025.

Dar es Salaam. Uzalishaji wa zao la shayiri nchini, ambalo ni malighafi muhimu katika utengenezaji wa bia, umeelezwa kuwa unachochea ukuaji na kuongeza uzalishaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), huku kinywaji cha Konyagi kikiongoza mauzo ya kampuni hiyo mwaka 2025.

Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa 53 wa Wanahisa wa TBL jijini Dar es Salaam leo Alhamisi Julai 2, 2026, Mwenyekiti wa Mpito wa Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni hiyo, Balozi Ami Mpungwe amesema upatikanaji wa shayiri inayolimwa nchini umeimarisha uzalishaji wa bia kwa kuwa zao hilo ni malighafi muhimu katika sekta hiyo.

Amesema pamoja na mchango wa shayiri, uwekezaji uliofanywa na kampuni, ikiwemo kuanza kwa uzalishaji katika Kiwanda cha Kilimanjaro chenye uwezo wa kuzalisha tani 8,000 kwa mwaka, umechangia TBL kushika nafasi ya pili kimataifa.

"Pamoja na hali ya mazingira magumu, Kampuni imeendelea kujiimarisha, ikishika nafasi ya pili kimataifa katika uzalishaji na usambazaji wa bia, huku tukihimili ushindani kutokana na kuongeza wigo wa ubunifu wa bia zinazotiwa ladha tofautitofauti," amesema.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Fedha wa TBL, Avito Swai amesema mauzo ya kampuni yaliendelea kuimarika mwaka 2025 huku Konyagi ikiwa bidhaa iliyoongoza kwa mauzo.

"Mwaka 2025 mauzo ya bia yalipanda hadi kufikia wanunuzi 22,000 na wasambazaji 15,000, huku Konyagi ikiongoza mauzo hayo," amesema Swai.

Amesema mwenendo huo unaonyesha kuendelea kuimarika kwa biashara ya kampuni, ambayo pia inaendelea kushikilia takribani theluthi mbili ya soko la bia nchini.