Wakulima wa mwani kicheko

Siwema Mohamed mkulima wa zao la Mwani kutoka katika Kijiji cha Mnazi kata ya Nalingu Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara alitoka kuvuna Mwani baharini. Florence Sanawa

Muktasari:

  • Baada ya kulilia soko kwa miaka 17, wakulima wa zao la Mwani wamepata wanunuzi watatu wa bidhaa hizo ambapo bei ya zao hilo imepanda kutoka Sh500 kwa Mwani mdogo hadi 1000 na kutoka 1000 kwa mwani mkubwa hadi kufikia 2000.

Mtwara. Kufuatia wakulima wa zao la Mwani kutoa kilio chao juu ya bei kuwa ndogo na mnunuzi kuwa mmoja huku akipanga bei kwa miaka 17 sasa wamepata wanunuzi zaidi ya watatu.

 Mwani ina uwezo wa kutengeneza bidhaa mbalimbali sabuni, mafuta, visheti juice soda mapambo dawa pia chakula kama tukiweza kuiambia jamii tunaweza kuwa na soko kubwa zaidi na kuongeza uzalishaji zaidi.

Akizungumza na Mwananchi, Tukae Magongo, mkulima wa zao la mwani kutoka katika kijiji cha Mnazi kata ya Nalingu alisema wamekuwa kifungoni kwa miaka 17 ambapo mnunuzi alikuwa mmoja na anapanga bei yake.

“Biashara ilianzia Sh500 mpaka 1000-1300 na sasa Sh2,000 hii inatunufaisha kwa kuwa hata ukiwa na kidogo unauza unapata pesa hali ya soko sio mbaya, tunao wanunuzi watatu sio sawa na mmoja aliyekuwa akinunua hapo awali,” amesema

Nae Shakifu Kambwili Mkazi wa Kijiji cha Mnazi alisema anashawishika kuanza kulima zao hilo kwakuwa sasa anaona hata mkulima akiwa na kilo mbili anapima na kupata pesa sio kumsubiri boss aje.

Mwenyekiti wa serikali ya Kijiji cha Mnazi, Faume Mchinji  alisema kupanda kwa bei ya mwani ni msaada mkubwa  kwa wakulima wa  zaod hilo ambapo saasa watapata pesa na kununua vifaa vinavyofaa vinvyotumika kwenye zao hilo.  

Nae Mustapha Kwiyunga, Mratibu wa shirika lisilo la kiserikali la Mtwara Society Against Poverty (Msoapo) alisema mpaka sasa vipo vikundi 30 vinavyozalisha zao la mwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara.

“Awali waliuza mwani mdogo 500 na mwani mkubwa 1000 na mnunuzi alikuwa mmoja tulijitahidi kutangza ambapo sasa tumepata wateja 3 na wanauza kutoka 500-1000 na kutoka 1000 mpaka 2000 mnunuzi alikuwa mmoja kwa miaka 17 na bei alikuwa anapanga yeye.”