Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tume ya Warioba ilivyoendesha nchini mchakato wa katiba

Jaji Warioba (kulia) akiwa kwenye mojawapo ya mikutano yake ya kukusanya maoni yenye lengo la kupata Katiba Mpya. Picha ya Maktaba.

Muktasari:

  • Aprili 6, 2012 saa 06:57 mchana, taarifa inayotaja majina ya wateule wa Rais katika kuunda tume hiyo inayoongozwa na Jaji, Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania, Joseph Warioba iliwekwa kwenye ukurasa mtandao wa kijamii wa face book, wa Rais Jakaya Kikwete.

 

Jumanne wiki hii, zilipatikana taarifa kwamba Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilikamilisha kuboresha rasimu ya kwanza na kupata rasimu ya pili ya Katiba Mpya. Naibu Katibu wa tume hiyo, Casmir Kyuki alithibitisha hayo.

Mwanzo wa Tume

Aprili 6, 2012 saa 06:57 mchana, taarifa inayotaja majina ya wateule wa Rais katika kuunda tume hiyo inayoongozwa na Jaji, Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania, Joseph Warioba iliwekwa kwenye ukurasa mtandao wa kijamii wa face book, wa Rais Jakaya Kikwete ukisomeka:-

Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba (Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura 83, Toleo la 2012, Vifungu 5, 6 na 7).

Uongozi wa Juu

1. Jaji Joseph Sinde Warioba - Mwenyekiti

2. Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani - Makamu Mwenyekiti.

Wajumbe kutoka  Bara

1. Profesa Mwesiga L. Baregu

2. Riziki Shahari Mngwali

3. Dr. Edmundi Adrian Sengodo Mvungi

4. Ndugu Richard Shadrack Lyimo

5. Ndugu John J. Nkolo

6. Alhaj Said El-Maamry

7. Ndugu Jesca Sydney Mkuchu

8. Profesa Palamagamba J. Kabudi

9. Ndugu Humphrey Polepole

10. Ndugu Yahya Msulwa

11. Ndugu Esther P. Mkwizu

12. Ndugu Maria Malingumu Kashonda

13. Mheshimiwa Aly-Shymaa J. Kwegyir (MB)

14. Ndugu Mwantumu Jasmine Malale

15. Ndugu Joseph Butiku

Uongozi wa Sekretarieti

1. Assa Ahmad Rashid - Katibu

2. Casmir Sumba Kyuki - Naibu Katibu

Ilielezwa kuwa tarehe rasmi ya kuanza kazi ingetolewa baada ya wajumbe wote kujulishwa juu ya uteuzi na baadaye kuapishwa. Kisheria tume ilipaswa kuwa imekamilisha kazi yake ndani ya miezi kumi na minane (18).

Idadi ya Wateule wa Rais walioanza kazi pamoja yapungua

Dk Sengondo Mvungi alifariki dunia kufuatia kushambuliwa usiku akiwa nyumbani kwake; alijeruhiwa  na hatimaye kupoteza maisha akiwa nchini Afrika ya Kusini alikopelekwa kwa ajili ya matibabu. Mungu aiweke Roho yake, mahali pema peponi.

Rasimu ya pili ya Katiba Mpya ya Tanzania imekamilika, kinachosubiriwa ni siku ambayo tume itaikabidhi kwa Rais Kikwete, tukio linalotarajiwa kufanyika hadharani.

Mengi yamejiri wakati tume hii ikiwa kazini, changamoto nyingi zimetokea na mengi yameamuriwa na kutekelezwa.

Miongoni mwa mambo yaliyovuta hisia za wengi ni hoja iliyowasilishwa bungeni na Mbunge wa Kisarawe, Seleman Jafo, akitaka tume hiyo ivunjwe mara baada ya rasimu ya pili kuwasilishwa kwa Bunge Maalumu la Katiba.

Baada ya vuta nikuvute iliyoendelea Bungeni na kuibua mjadala hata nje ya Bunge, hatimaye ilikubaliwa kwa kupitishwa kisheria kuwa tume ya mabadiliko ya Katiba haitaingia kwenye Bunge maalumu la Katiba na itavunjwa kama hoja ya Jafo ilivyopendekeza.

Akizungumzia uamuzi huo wa Wabunge, Casmil Kyuki ambaye ni Mwandishi Mkuu wa Sheria nchini anasema wanaafikiana na uamuzi huo na kwamba wanauona umewaepushia shari. “Kila kitu maishani kina uzuri na ubaya wake, tungewasaidia ndani wa kamati, lakini wangeweza kufanya tofauti kwenye mijadala bungeni ambako tusingekuwa na uwezo wa kuchangia wala kutoa ufafanuzi wowote,” anaeleza Kyuki.

Msimamo huo ulitolewa na Wabunge wakidai pamoja na mambo mengine kuwa uwapo wa tume hiyo ndani ya vikao vya Bunge maalumu la Katiba, ungewabana.

Anasema ni heri ikitokea kazi yao ikaharibiwa, iwe hivyo bila wao kuwapo. Anasema ingewaumiza sana endapo kazi iliyowagharimu mambo mengi, ingefanyiwa tofauti huku wakishuhudia na wakiwa hawana uwezo wa kufanya lolote.

Baadhi ya Watanzania wana hofu kwamba huenda mchakato wa kupata Katiba Mpya Bungeni ukamezwa na chama chenye vyama vingi, badala ya matakwa thabiti ya wananchi.

“Nina wasiwasi mahitaji ya wananchi hayatazingatiwa, watajali zaidi matakwa yao hasa yale ya kisiasa,” anasema Mama Shila Mgono katika mahojiano na mwandishi wa makala haya.

Mama Mgono ambaye ni mfanyabiashara katika maeneo ya Kariakoo, anasema ni suala la msingi sana kwa wabunge nchini na wale wote wenye mamlaka kufanya kazi kwa kujali maslahi ya taifa, badala ya chama au mtu fulani. Akasisitiza kuwa katika taifa changa kiuchumi kama Tanzania likiweka sheria nzuri, uchumi utakuwa kwa kasi kubwa. Watanzania wengi wanaonekana kuwa na shauku kubwa na kuiona Katiba Mpya.