20 wahofiwa kuzama majini baada ya meli kugonga daraja Marekani

Marekani. Idara ya zimamoto na uokoaji ya Jiji la Baltimore nchini Marekani, imesema watu 20 wanahofiwa kuzama majini baada ya daraja la Francis Scott lenye urefu wa maili 1.6 (kilomita 2.57) lililopo Maryland, nchini humo kuanguka baada ya kugongwa na meli.

Hayo yameelezwa leo Jumanne Machi 26, 2024 na Kevin Cartwright, aliyezungumza na CNN kwa niaba ya idara hiyo.

"Inawezekana karibu watu 20 wanaweza kuwa katika Mto Patapsco hivi sasa, pamoja na magari mengi," amesema.

Video inayosambaa katika mitandao ya kijamii inaonyesha meli ikigonga daraja, baada ya hapo sehemu kubwa ya daraja hilo likaanguka kwenye Mto Patapsco.
Endelea kufuatilia katika mitandao yetu