Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bibi kizee acheza rhumba katikati ya mazishi

Francesca Ingosi akicheza mziki wa Rhumba.

Muktasari:

  • ‘Raha jipe mwenyewe usisubiri kupewa’ ni msemo unaoweza kuutumia baada ya bibi kizee kucheza na kuimba kwa bashasha katika mazishi.

Kongo. Bibi kizee Francesca Ingosi wa nchini Kongo, amekuwa kivutio msibani baada ya kusakata rhumba kwenye msiba wa ndugu yake, jambo ambalo limeibua mjadala kwa watu waliokuwa wameshiriki shughuli hiyo kutokana na maeneo mengi kama hayo watu kuwa na nyuso za huzuni.

Mtandao wa TUKO wa nchini Kenya umeeleza kwamba, jirani na eneo yalipokuwa yanafanyika mazishi, ulipigwa muziki wa rhumba uliomfanya Francesca kushindwa kujizuia na kuanza kuimba na kucheza kwa bashasha kwa sababu ya kufahamu lugha ya Kilingala.

Kutokana na kioja cha bibi huyo ambaye hakujali umati uliokuwepo, baada ya shughuli ya mazishi wahusika wa sehemu ambako muziki  huo wa Kilingara ulikuwa ukisikika walilazimika kumkaribisha nyumbani baada ya kushuhudia tukio hilo.

"Baba yangu alikuwa msimamizi hapa Kitale, na tulikuwa tukikaa karibu na ukumbi wa kijamii ambapo wasanii wa Lingala walikuwa wakitumbuiza, kisha tunarudi na kulala nyumbani kwetu." Alisimulia bibi huyo akikumbuka chanzo cha kujikuta akicheza wimbo huo.

 Tukio hilo limeibua hisia mbalimbali kwa watu wengi ikilichukilia kuwa sio utamaduni wa Waafarika kuanza kucheza nyimbo za furaha wakati shughuli za msiba zikiendelea.