Bill Gates, mkewe waachana baada ya miaka 27 ya ndoa

Tuesday May 04 2021
bill pccc

Tajiri namba nne duniani kwa mujibu wa jarida ya Forbes, Bill Gates na mkewe, Melinda wametangaza talaka yao baada ya miaka 27 ya ndoa.

“Hatuamini tena tunaweza kuwa pamoja kama wanandoa. Baada ya kufikiria sana na kufanya kazi nyingi juu ya uhusiano wetu, tumefanya uamuzi wa kumaliza ndoa yetu," wameeleza wawili hao waliokutana kwa mara ya kwanza mwaka 1980.

Melinda aliyejiunga na kampuni ya Bill ya Microsoft mwaka 1980 na Gates wana watoto watatu.

Bill Gates ni tajiri namba nne duniani kwa mujibu wa jariba la Forbes na utajiri wake ulianza mwaka 1970 kupitia kampuni ya Microsoft.

bill pcc

“Katika kipindi cha miaka 27 iliyopita tumewalea watoto watatu wa ajabu na kujenga wakfu ambao unafanya kazi ulimwenguni kote kuwezesha watu wote kuishi maisha yenye afya, yenye tija.”

Advertisement

"Tunaendelea kuwa na imani ya pamoja katika lengo hilo na tutaendelea kufanya kazi pamoja kwenye wakfu wetu  lakini hatuamini tena tunaweza kukua pamoja kama wanandoa katika sehemu inayofuata ya maisha yetu.

bill pc

Tunaomba nafasi na faragha kwa familia yetu tunapoanza maisha haya mapya,” wameeleza kupitia mtandao huo.

Advertisement