Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kauli za waziri mkuu wa Pakistan zazua jambo

Muktasari:

  • Kauli za shutuma dhidi ya nchi za Ulaya zilizotolewa na waziri mkuu wa Pakistan, ziliathiri mazungumzo  hali iliyosababisha Uingereza kusitisha mikutano yao miwili muhimu.

Kauli za shutuma dhidi ya nchi za Ulaya zilizotolewa na waziri mkuu wa Pakistan, ziliathiri mazungumzo  hali iliyosababisha Uingereza kusitisha mikutano yao miwili muhimu.

Machi 6 ,2022 Khan alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara katika mji wa Vehari huko Punjab Kusini alisema wanadiplomasia wa Magharibi waliifanya Pakistan kama watumwa kwa kushinikiza kuwa na msimamo mkali zaidi kuhusu Urusi juu ya mgogoro wa Ukraine.

Pia aliwakashifu wajumbe wa Umoja wa Ulaya kuhusu barua yao ya kutaka Pakistan kubadili msimamo wao wa kutoegemea upande wowote  kuhusu kile kinachoendelea Ukraine.

Wachambuzi wanasema Khan anajenga hisia dhidi ya nchi za magharibi  ili kupambana na mzozo wa kisiasa ambapo upinzani umetoa notisi ya kuwasilisha hoja ya kutokuwa na imani na serikali katika Bunge la Kitaifa.

Kulingana na baadhi ya ripoti za vyombo vya habari, Khan na wenzake wamekuwa wakidai kuwa Marekani ndio wanaohusika na hatua ya Bunge kumwondoa madarakani.

Chanzo cha Serikali ya Uingereza ambacho hakikutajwa jina Machi 9, 2022 kilinukuliwa na gazeti la The News International kikisema kwamba kulaani hadharani kwa Waziri Mkuu Imran Khan kwa mataifa ya Ulaya kumesababisha hali ya wasiwasi miongoni mwa nchi, hasa Uingereza, ambayo mara nyingi imekuwa ikiunga mkono Pakistan katika vikao mbalimbali vya kimataifa.

Lugha ya Khan dhidi ya nchi za Ulaya imeikasirisha Marekani pia, tangu ilipojitoa kwa ghasia kutoka nchi jirani ya Afghanistan Agosti uliopita.

Amezilaumu nchi za Ulaya na Marekani kwa ujumla kwa kulazimisha Pakistani kujiunga na vita dhidi ya ugaidi nchini Afghanistan baada ya miongo miwili iliyopita.

Jambo la kuvutia zaidi kwa Pakistan ni kuhairishwa kwa majadiliano  kuhusu hali ya Afghanistan.

London inadaiwa kusitisha mwaliko kwa mshauri wa usalama wa kitaifa, Dk Moeed Yusuf na ziara ya mapfisa wakuu ili kujadili miongoni mwa mambo mengine, usaidizi kwa Pakistan na hali ya Afghanistan.

Mwaliko kwa Moeed ulitoka kwa mshauri wa usalama wa kitaifa wa Uingereza, Stephen Lovegrove.

Moeed alikanusha kughailishwa kwa mkutano huo na kudai kuwa alikuwa na mazungumzo kwa njia ya mtandao na mwenzake wa Uingereza na kuhutubia kwa njia ya Zoom.

 Wakati wa hotuba yake, NSA ya Pakistani ilisema kuwa taarifa za kusitishwa kwa mkutano kati yake na  Serikali ya Uingereza si za kweli.

 Kulingana na ratiba yake ya awali, alitakiwa kukutana na Mshauri wa masuala ya  usalama wa kitaifa wa Uingereza, mawaziri wakuu katika ofisi ya mambo ya nje na pia mkutano na ofisa mkuu wa Jeshi la Uingereza katika ziara yake ya siku nne, ikiwa ni pamoja na kuhutubia katika Shule ya Uchumi ya London (LSE) tukio linalofanywa kila mwaka na Pakistan Society.

Pakistan inajiona kama mwezeshaji na mratibu wa misaada ya kibinadamu kwa Afghanistan.

Hatua ya kufungua akaunti ya benki ya kimataifa ambayo  misaada hiyo ya kimataifa inaweza kupitishwa imekataliwa na wadau mbalimbali.

Kupitia juhudi hizo, Pakistan pia inatarajia kupata ahueni kwa mamilioni ya wakimbizi wa Afghanistan ambayo imekuwa ikiwahifadhi, baadhi yao kwa zaidi ya miongo minne.

Ripoti za vyombo vya habari zinasema kuwa kutokana na wakimbizi wa Ukraine kusambaa katika maeneo mbalimbali ya Ulaya, matarajio ya Waafghan kupata hifadhi katika maeneo ya Ulaya na Marekani yamefifia.