Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kiongozi mkuu kundi la Hamas auawa Iran

Kiongozi Mkuu wa Kundi la Hamas, Ismail Haniyeh. Picha na Mtandao

Muktasari:

  • Kiongozi Mkuu wa Hamas, Ismail Haniyeh, amefariki dunia baada ya kuvamiwa akiwa nyumbani mjini Tehran.

Kiongozi Mkuu wa Kundi la Hamas, Ismail Haniyeh amefariki dunia leo Julai 31, 2024 alipovamiwa kwenye makazi yake mjini Tehran, Iran.

Haniyeh ameuawa siku moja baada ya kushiriki sherehe za kuapishwa kwa Rais mpya wa Iran, Masoud Pezeshkian aliyeapishwa jana Jumanne.

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Iran (The Iranian Revolutionary Guard Corps) limesema chanzo cha tukio hilo bado hakijafahamika na wanaendelea uchunguzi.

Haniyeh (62), alikuwa mwanachama mashuhuri wa Hamas mwishoni mwa miaka ya 1980. Alichaguliwa kuwa mkuu wa Kundi la Hamas mwaka 2017.

Taarifa za kifo cha Haniyeh, zimeripotiwa muda mfupi tangu Israel itangaze kumuua kamanda wa Hezbollah ikidai ndiye aliyehusika na shambulio katika milima ya Golan na kuisababisha Israel kurudi nyuma kuhusu makubaliano ya kusitisha mapigano huko Gaza.


Endelea kufuatilia Mwananchi