Sekta ya zao la pamba yakumbwa na misukosuko Pakistan

Muktasari:

Vyombo mbalimbali vya habari vimeripoti kuhusu nchi ya Pakistan inavyopambana kuongeza akiba yake ya fedha za kigeni inayopungua.

Vyombo mbalimbali vya habari vimeripoti kuhusu nchi ya Pakistan inavyopambana kuongeza akiba yake ya fedha za kigeni inayopungua.

Ripoti imemnukuu mwenyekiti wa All Pakistan Textile Mills Association (APTMA),  Hamid Zaman akisema kuwa wafanyakazi na wafanyabiashara wa viwanda vya nguo wanaweza kuandamana ikiwa serikali haitazuia pamba iliyoagizwa kutoka nje.

"Mwaka huu, mauzo ya nguo yatapunguzwa hadi dola bilioni 16-17," amesema Zaman.

Ripoti ya Geo News inaeleza kuwa kuna uagizaji wa  pamba ghafi kutoka nje na baada ya kuongezwa thamani inasafirishwa nje ya nchi kwa bei ambayo ni  mara nne ya thamani iliyoagizwa huku serikali ikitakiwa kuruhusu wauzaji bidhaa kuagiza nje kwa asilimia 35 ya thamani ya mauzo.

Mkuu wa APTMA alionya kuwa watu milioni saba wanaohusishwa na sekta hiyo watakosa ajira mnamo Januari ikiwa mambo hayatadhibitiwa.

Takriban asilimia 30 hadi 50 ya viwanda vya nguo vilikuwa vimefungwa kabisa, amesema Zaman kulingana na ripoti hiyo.

‘’Malipo ya kupunguzwa na kuzuiwa kwa bidhaa zilizoagizwa kutoka nje yalikuwa yamezidi thamani ya bidhaa ambazo kampuni za kigeni zilipaswa kulipa, ‘’ amesema Zaman.