Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bomu lalipukia watoto, wajeruhiwa

Muktasari:

Wiki iliyopita msitu huo uliopo wilayani Geita, ulitumiwa na askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kufanya mazoezi ya kijeshi.

Geita. Watoto wawili wamejeruhiwa kwa bomu la kutupa kwa mkono katika Msitu wa Kanyala wilayani hapa, walikokwenda kutafuta kuni.

Wiki iliyopita msitu huo uliopo wilayani Geita, ulitumiwa na askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kufanya mazoezi ya kijeshi.

Akizungumza jana, mtoto Frank Salim (14) aliyeumia miguuni kutokana na mlipuko wa bomu alisema akiwa na rafiki yake,  Yohana Alex (18) walikwenda msituni kuokota kuni.

Alisema Alex aliokota bomu hilo na alitaka kuligonga kwenye jiwe, lakini akamtahadharisha asifanye hivyo, wakati wakibishana lililipuka na kumjeruhi mwenzake tumboni na yeye miguuni.

 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo alisema tukio hilo lilitokea juzi jioni na kwamba chuma cha bomu hilo kilimjeruhi mtoto mmoja na kuingia tumboni na hali yake ni mbaya.

Mbunge wa Geita Mjini, Constantine Kanyasu aliyewatembelea watoto hao waliolazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Geita aliomba JWTZ kuondoa mabomu yaliyosalia msituni na Serikali kubeba gharama za matibabu ya watoto hao.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Geita,  Dk Brian Mawala alisema aliwapokea watoto hao juzi saa 11:00 jioni na kwamba, Alex amefanyiwa upasuaji baada ya kubainika bandama lilipasuka na hali yake inaendelea vizuri.